Hakimi na Ex wake waonekana pamoja

Hakimi na Ex wake waonekana pamoja

Nyota wa Paris Saint-Germain (PSG) Achraf Hakimi (25) na aliyekuwa mkewe mwigizaji Hiba Abouk (37), wameripotiwa kuonekana pamoja kwa mara ya kwanza baada ya kupeana talaka mwaka jana.

Kwa mujibu tovuti ya ‘Sports Ration’ imeeleza kuwa wanandoa hao wa zamani walionekana kwenye moja ya mgahawa ulipo Hispania wakiwa na watoto wao wawili Amin na Naim, huku ikidaiwa kuwa walikutana kwa lengo la kuzungumza kuhusiana na mustakabali wa watoto wao.

Wakati wa mazungumzo yao wanandoa hao wa zamani hawakuwepo peke yao kwani alikuwepo nyota wa Real Madrid, Kylian Mbappé jambo ambalo liliibua hisia tofauti kwa wadau mbalimbali katika mitandao ya kijamii huku sababu ya kikao cha watatu hao bado hakijawekwa wazi.

Utakumbuka kuwa talaka ya wawili hao ilizua gumzo kupitia mitandao ya kijamii baada ya Hiba Abouk, kutaka mali alizokuwa nazo Hakimi na kubainika kuwa nyota huyo anayekipiga katika timu ya PSG hana utajiri wowote kwani pesa anazozipata zote zinakwenda kwa mama yake mzazi.

Hakimi (25) ana zaidi ya utajiri wa Dola milioni 24, sawa na Sh56.2 bilioni ingawa asilimia 80 ya mshahara wake anaolipwa kwa mwezi unaingia moja kwa moja kwenye akaunti ya benki ya mama yake.

Hiba Abouk na Hakimi walifunga ndoa mwaka 2020 na wamefanikiwa kupata watoto wa kiume wawili Amin na Naim.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags