Gym  za bure Mitaani nchini India

Gym za bure Mitaani nchini India

Suala la ufanyaji mazoezi limekuwa  likisisitizwa sana kwa jamii lengo ikiwa ni kuimarisha mwili ili kuondokana na baadhi ya magonjwa, kwa upande mwingine inaonekana baadhi ya vijana wamekuwa wakitumia muda wao kufanya mazoezi gym na wale wasiokuwa na pesa ya kulipia gym basi hutumia mbinu mbalimbali ili tu kupasha miili yao.

Hivi umewahi kufikiria vipi kama kila mtaa ukawekewa gym za bure ambazo watu watakuwa wakifanya mazoezi bila malipo yoyote? Nchini India suala hilo sio la kufukiria tena kwa sababu katika maeneo mengi ya jiji ‘Manispaa’zimewekwa sehemu za kufanya mazoezi ya viungo bure bila malipo yoyote.

 Jambo hilo limekuwa msaada hata kwa wale ambao hawana pesa za kulipia gym, kwenda katika maeneo hayp kufanya mazoezi bila uwoga wowote kwani huduma wanayopata haiwasumbui kimalipo.

Siku ukipata bahati ya kukatiza kwenye maeneo mbalimbali nchini India usishangae kukutana na watu wakifanya mazoezi maeneo mbalimbali, kwani wazee vijana na watoto wote hujumuika kwa pamoja.

Katika kila eneo la gym limewekewa zaidi ya vifaa 15 kwa ajili ya mazoezi pamoja na mwalimu wa kufundisha namna ya kufanya mazoezi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags