Gwiji la soka Pele afariki dunia

Gwiji la soka Pele afariki dunia

Gwiji wa timu ya taifa ya Brazil Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pelé (82), amefariki Dunia jana usiku katika Hospitali akiwa anapatiwa matibabu ya moyo pamoja na Cancer .

Pele alilazwa Novemba 29, 2022 baada ya hali yake kuonekana kuwa mbaya sana lakini alikuwa chini ya uangalizi maalumu wa madakatari tangu Septemba 2021.

Dunia itamkumbuka Pele kama mchezaji mdogo kuwai kushinda kombe la Dunia mara mbili mfululizo (1958, 1962 ) kabla ya kushinda tena baadae (1970) na kuwa mchezaji pekee aliyeshinda ubingwa wa Dunia mara tatu.

Rekodi yake nyingine ni kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa fainali akiwa na miaka 17 na siku 249 , hadi anafariki anashikilia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote wa Brazil akiwa na mabao 77 kwenye mechi 92.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags