Grace Gumanga: Biashara ya vipodozi inaikomboa familia yangu

Grace Gumanga: Biashara ya vipodozi inaikomboa familia yangu

Na Aisha Lungato

Ni Jumanne nyingine tena tunakutana nikiwa na matumaini makubwa kuwa uko poua mwanangu mwenyewe unayefuatili jarida hlili la Mwananchiscoop.

Siku kama ya leo ambayo tunaangazia Makala za biashara basi tumekuwa tukikuletea wanafunzi wanaosoma lakini huku wanajishuhulisha na biashara mbalimbali kwa lengo la kukidhi mahitaji yao.

Najua tumeshazoe kusikia wanafunzi wengi wanafanya biashara kwa ajili ya mahitaji yao madogo madogo lakini kwa wengine imekuwa tofauti sana kwasababu biashara hizo ndizo zinazo emdesha maisha yao kwa ujumla kama vile kulipa kodi, kulipa ada na kusaidia familia yake kwa matatizo mbalimbali.

Grace Gumanga ni mwanafunzi kutoka katika chuo cha uandishi wa habari cha Dar es Salaam School of Journalism (DSJ) anayesomea masomo ya journalism na kwa sasa yupo mwaka wa pili.

Licha ya kuwa ni mwanafunzi lakini maekuwa akijishugulisha na biashara ya kuuza vipodozi mbalimbali kama vile mafuta ya kupaka, pafyum na cream mbalimbali za kurainisha ngozi na kutakatisha.

KWANINI ALIAMUA KUFANYA BIASHARA HIYO

Mwanadada huyo anasema kuwa aliamua kufanya biashara hiyo ya vipodozi ni kwa sababu inalipa na hiyo ni kutokana kupendwa na wadada wanaopenda kuwa na ngozi nzuri.

“Niliamua kufanya biashara ya vipodozi kwa sababu inanilipa sana na nikwambie kuwa ikitoka biashar ya chakula inafuatia hii ya vipodozi kwa kulipa.

“Na hii hali inatokana na wadada wengi na wamama kupenda kuwa na ngozi nzuri hivyo wakipata kitu kizuri original basi hawana budi kukinunua hata kiwe kinauzwa kiasi gani, cha muhimu tu katika biashara hii ni kuhakikisha unakuwa na vitu vilivyobora,” alisema mrembo huyo.

Aliongezea kwa kusema “Wazo la biashara ya vipodozi lilikuja baada ya watu wengi kuniuliza kuhusu ngozi yangu na rangi yangu nikaichukulia kama fursa kwangu”

BIASHARA IMEKUWA MKOMBOZI

Hata hivyo Grace anatambua kuwa katika biashara kumekuwa na  faida na hasara hiyo amefunguka na kusema amekuwa akipata faida na imekuwa ikimsaidia kulipa kodi, ada ya chuo na kukidhi mahitaji yake ya kila siku.

“Naweza kusema biashara hii imekuwa mkombozi katika familia yangu, kwani imeweza kuwapunguzia baadhi ya majikumu kwani faida ninayoipata ndiyo inatumika kunilipia ada ya chuo, kulipa kodi mahali ninapoishi na mahitaji mengine,” alisema

KUHUSU CHANGAMOTO

Tunafahamu kuwa katika kila biashara kumekuwa na changamoto na hazionekana hivyo Gumanga anafunguka na kusema moja ya changamoto anayokutana nayo ni baadhi ya wateja wake kukopa vitu.

“Changamoto ninayokutana nayo kwenye biashara yangu ni mikopo kwa sababu lazima watu wakope, na wakishakopa wengine wanakuwa wasumbufu kulipa mpaka mzungushane ndipo mtu aamue kulipa “alisema Gumanga

AWASHAURI VIJANA

Mrembo huyo ametoa ushauri kwa vijana wenzake ambao hawajishuhulishi na kueleza kuwa “Nawashauri vijana wasibweteke wachangamkie fursa zinazotokea mbele yao ili kutengeneza maisha bora kwao na familia zao, pia watumie vipaji vyao kuwapatia pesa na kukidhi mahitaji yao madogo madogo” alisema Gumanga

ANACHOKIPENDA KINGINE KUFANYA

Nje ya masomo na kufanya biashara kuna kile kitu ambacho kila mtu anacho anakiota kila siku na kukipenda kukifanya wengine hupendelea mpira, kudance, kuimba kwa upande wa mrembo yeye alieleza kuwa kitu anacho kipenda na anacho kiota kila siku ni kujakuwa mtangazaji bora hasa wa habari na burudani.

“Napendelea kutangaza haswa vipindi vya habari na burudani lakini pia matamanio yangu siku moja nije kuzalisha vipodozi vyangu mwenyewe na niwe na kampuni yangu ambayo itazalisha vipodozi hivyo,” alisema

Aidha Vijana na mabinti wengi siku hizi hupendelea zaidi kutembelea nyayo za mtu au watu  ambao washapata mafanikio kwa namna moja ama nyingine, kwa mrembo Grace yeye role model wake ni mtangazaji machachari sana anaejulikana nje na ndani ya Tanzania na huyu si mwingine ni Zuhura Yunus ambae ni mtangazaji wa BBC.

Binti huyo alifunguka na kisema kuwa anatamani kuwa kama Zuhura Yunus kwa sababu ni mtangazaji ambaye alianza kumfatilia tangu akiwa mdogo.

“Napenda sana anavyo tangaza na umakini katika utangazaji wake, hivyo basi na mimi natamani kuwa mtangazaji mkubwa ndani na nje ya nchi,” alisema

Haya haya mdau na mfuatiliaji wa @mwananchischoop funguka hapo chini wewe unatamani kuwa kama nani eeeeh, umejifunza nini kutoka kwa mwanadada Grace.

Au tuambie unatamani kufanya biashara gani lakini mazingira hayakuruhusu kwa namna moja ama nyingine usiache kufuatilia magazine ya @mwananchisoop ili uweze kujifunza mbinu mbalimbali za kibiashara.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags