Na Habiba Mohamed
Ukisubiri upate mtaji wa rasilimali fedha, ndipo uanze kufanya biashara basi unaweza kuchelewa sana au kutofanya kabisa.
Biashara nyingi sio mpya, nyingi ni mwendelezo wa zile zilizoanzishwa (kwa lugha nyepesi za urithi).
Kwa sababu asili yetu ilikuwa katika mfumo wa ujamaa, hivyo maswala mengi yalifuata mfumo wa kushirikiana na kugawana sawa sawa.
Hivyo suala la biashara liliendeshwa kiujamaa. Biashara nyingi zimeanza kufanyika mwishoni mwa miaka ya 80’s kiasi ambacho ilikuwa ngumu sana kuanza maana Sanaa ya biashara ilikuwa ni somo jipya sana.
Leo katika Makala yetu nimekusogezea kijana mtanashati kwa majina anaitwa Samuel Mgobi maarufu kama Godyndevu.
Kijana Gobyndevu ambaye anasoma Chuo cha Institute of Social Work akichukua kozi ya Business Administration mwaka wa 3, ameamua kujikita katika uuzaji wa biashara wa bidhaa za kiume.
Gobynndevu ambaye aliona fursa ya kuanzisha biashara hiyo ya uzalishaji na uuzaji wa men product ambazo ni mafuta ya kukuza na kuboresha afya ya ndevu, ya nywele, shampoo, conditioner, scrub pamoja na face cleansers.
Alisema wazo la kuanzisha biashara hiyo lilikuja kutokana na kutopenda namna alivyokuwa akipatwa na vipele baada tu ya kunyoa ndevu zake.
“Hivyo kupitia changamoto hiyo ilinilazimu nisome online ili nijifunze kwa kina na kupata suluu ya afya ya ngozi, ndevu na nywele kwa kutumia vitu asilia kupitia application ya Asilispot.
“Ambapo nilijifunza kutengeneza bidhaa zangu hizo kwa kutumia mbegu za mimea kama fengreek seed, rose petals pamoja na essential oil for infusion,” alisema.
Alisema Godyndevu product imelenga kuondoa changamoto kwa wanaume wote wenye ndevu ambao wanaosumbuliwa na muwasho kabla au baada ya kunyoa ndevu au nywele na hata wale wasio na ndevu kwani mafuta ni mazuri pia kwa matumizi ya nywele.
Aidha alisema pamoja na kufanya kazi hiyo yapo mafanikio aliyojaaliwa kuyapata na miongoni mwao ni kumiliki page Instagram.
Alisema pia amefanikiwa kutoa elimu kuhusiana na afya ya ngozi, ndevu na nywele pia kuweza kuleta utatuzi kwa baadhi ya watu waliokuwa wakisumbuliwa na changamoto ya ngozi.
“Vilevile unakuta nina product unakuta wateja wanataka kuzichukua bidhaa kwa usu bei ili kama itawasaidia ndipo wamalize fedha inayobakia,” alisema
Alisema wapo wateja wengine ambao ukimbia kabisa mara baada ya kutrumia bidhaa na kushindwa kuilipia kwa kigezo kutaka kuona matokeo yake.
“Wengine bwana unakuta amechukua bidhaa alafu anakimbia kabisa na deni, so inakuwa hasara kwangu, ila Mungu ni mwema mdogo mdogo kazi zinasonga, ipo siku tutafikia yale tunayoyatamani kufikia,” alisema
Aidha alisema analipongeza jarida la MwananchiScoop kwa kuangazia vijana wa vyuo vikuu na kupiga nao story za hapa na pale kwa lengo la kujifunza vitu mbalimbali na kutazama changamoto zinazowakabili na kuzifikisha mamlaka uhusika.
“Napongeza jitihada za Mwananchi scoop kuandaa hili jarida kwa ajiri ya wanafunzi tuliyopo chuoni kuweza kungarisha vipaji vyetu pamoja na biashara, hivyo basi wanafunzi wenzangu tutumie nafasi hii kujihimarisha kwenye biashara zetu,” alisema.
Hata hivyo alisema Favourite Sport yake ni formula 1, Hobbies yake ni kusoma na kufanya uchunguzi wa kazi na habari mbalimbali.
Alisema pia moja ya ndoto zake za baadae ni kuja kuwa mjasilimali mkubwa ndani na nje ya nchi kupitia kazi zake za beauty industry.
STEVEN
Toka hapo mwanzo maisha yetu ni ya kutegemeana hvyo tunaendeleza tulichoachiwa kikubwa ni kuongezea ubunifu wa vitu tofauti tofauti. Pongezi kwake kwa kuliona hilo pia kwa Mwananchi scoop kwa kutambua hitaji la vijana kwa ujumla .