Gigy Money achoshwa na wanaodukua akaunti zake

Gigy Money achoshwa na wanaodukua akaunti zake

Mwanamuziki wa Bongofleva, Gift Stanford ‘Gig Money’, ambaye hivi karibuni alikutana na majanga ya kudukulia akaunti yake ya YouTube akizungumza na Mwananchi Scoop amekiri kuchoshwa na wanaomfanyia vitendo hivyo.

“Nimechoka kila siku mimi tu, wana-hack akaunti, natumia pesa nyingi kuwalipa watu wa kuirudisha, kisha inavamiwa tena! Kwanini? Nimechoka. Sasa hivi wala sijali na wala sitaki kumjua aliyefanya hivyo, nimeamua kuacha hili jambo, sina muda wa kulifuatilia kwa bashasha, nafuatilia kimyakimya tena nikiwa na muda ikirudi sawa, isiporudi sawa tu pia,” amesema mwimbaji huyo wa ngoma ya ‘Kiki ni Gigy’.

Hii siyo mara ya kwanza kwa msanii huyo kudukuliwa akaunti zake kwani mapema mwishoni mwa mwaka jana akaunti yake ya Instagram ilidukuliwa na aliyemuibia simu.

Licha ya kuzungumzia kuhusiana na kuchukuliwa akaunti zake pia ameeleza hali yake ya mahusiano kwa kudai haelewi kwa sasa kama yupo kwenye mahusiano au laa!.

“Mimi hata sijui kama nipo kwenye uhusiano, maana mpenzi niliye naye sasa haeleweki, mara tupo pamoja mara hatupo pamoja, kiufupi liuhusiano langu halieleweki au siko kwenye uhusiano,”amesema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags