Gift atamani kuwa Miss Tanzania

Gift atamani kuwa Miss Tanzania

Miss Kinondoni Gift Moureen, mlimbwende anayechipukia kwa kasi ameeleza kwa undani kuhusiana na safari yake ya urembo na kusema anataka kuona siku moja anatwaa taji la Taji la Miss Tanzania.

Gift ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akiwa kwenye mahojiano na Clouds Media, amesema alipenda urembo tangu akiwa mdogo.

“Safari yangu ilianza toka nikiwa mdogo, nilikuwa napenda sana mambo ya urembo wazazi wangu pia walikuwa wananisapoti kwa hiyo hata nilivyofika sekondari tulikuwa tunafanya mashindano ya urembo na nilishinda Miss Baobao na watu walikuwa wananijua, hivyo na nilipofika chuo nikaona ni wakati wangu sahihi wa kuanza safari ya kuwa Miss Tanzania,” amesema.

Aidha katika mahojiano hayo ameeleza kuhusiana na mitazamo hasi ambayo anakutana nayo kwenye jamii.
“Kwanza kabisa mimi huwa napenda kuzingatia mambo yangu sisikilizi maneno ya watu kwa sababu kama majaji wameona ninafaa hakuna mwingine anayeweza kusema sifai na ingekuwa hivyo, basi na mimi nisingekuwa hapa kwa hiyo sisikilizi sana maneno ya watu,” amesema mrembo huyo.

Wakati wa mahojiano hayo Gift aliongozana na Miss Tanzania 2020, Rosey Manfere ambaye alieleza magumu aliyoyapitia baada ya Miss World kuahirishwa.

“Shida haikuwa kwanini sikwenda Miss World, lakini watu mitandaoni walianza kunisema vibaya, nilipata shida sana, nilipata depression, mimi nilikuwa mtu wa hospitali kila siku, nilipata shida lakini nashukuru familia yangu ilikuwa karibu na mimi katika kila hatua,” amesema.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags