Gereza linalotoa huduma kama hoteli

Gereza linalotoa huduma kama hoteli

Imani na hadithi za watu wengi zinaeleza kuwa gerezani ni sehemu ya mateso na dhiki, lakini hii inakuwa tofauti kwa gereza maarufu kutoka Norway liitwalo ‘Halden Prison’ ambalo linalinganishwa na hoteli ya kifahari kutokana na muundo wake pamoja na huduma za kisasa.

Kwa mujibu wa tovuti ya Wealth gereza hilo limejengwa kwa pauni milioni 138 huku likishinda tuzo mbalimbali za gereza bora nchini humo.

Katika gereza hilo mfungwa anapewa chumba cha pekeyake cha kulala, kujipikia akitakacho, kujifunza ujuzi wowote autakao, kuvaa mavazi ya kawaida kama raia wengine, kucheza game, na kufanya shughuli kama yupo uraiani.

‘Halden Prison’ lilipokea wafungwa wake wa kwanza Machi 1,2010 na lilifunguliwa rasmi Aprili 8 mwaka huo huo na Mfalme wa Norway Harald V. Ni gereza la pili kwa ukubwa nchini Norway lenye uwezo wa kuchukua wafungwa 248-252.

Ili kutumikia kifungo katika gereza hilo kila mfungwa anatakiwa kulipa takriban £98,000 kwa mwaka ambapo mpaka kufikia sasa linatajwa kuwa na zaidi ya wafungwa 250.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post