Gavana Taliban auwawa kwenye Shambulio

Gavana Taliban auwawa kwenye Shambulio

 

Gavana wa Taliban wa jimbo la Balkh kaskazini mwa Afghanistan ameuawa katika shambulio la kujitoa mhanga linalodaiwa na kundi la Islamic State (IS).

Mohammad Dawood Muzammil aliuawa katika ofisi yake katika mji mkuu wa mkoa, wa Mazar-e Sharif, siku ya Alhamisi.

Ndiye afisa mkuu wa Taliban kuuawa tangu wanamgambo hao warejee mamlakani mwaka 2021.

Ghasia zimepungua sana tangu wakati huo, lakini maafisa wakuu wanaounga mkono kundi la taliban wamekuwa wakilengwa na IS.

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid alisema kwenye Twitter kwamba gavana huyo “aliuawa kama shahidi katika mlipuko wa maadui wa Uislamu”.

Muzammil alikuwa ameongoza vita dhidi ya IS katika wadhifa wake wa awali kama gavana wa jimbo la mashariki la Nangarhar Alihamishiwa Balkh Oktoba iliyopita.

Hata hivyo Msemaji wa polisi wa Balkh Mohammed Asif Waziri alisema mlipuko huo ulitokea Alhamisi asubuhi kwenye ghorofa ya pili ya ofisi ya gavana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags