Gardner afariki dunia

Gardner afariki dunia

Mtangazaji maarufu wa Redio ya Clouds FM, Gardner G Habash amefariki dunia, Msemaji wa Kampuni Clouds Media, Emilian Mallya amethibitisha.

Gardner aliyekuwa mtangazaji wa kipindi Jahazi, amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), leo alfajiri saa 11 April 20, 2024.

“Ni kweli kwa taarifa za awali amefariki dunia, lakini nitatoa taarifa zaidi baadaye,” amesema Mallya.

Kabla ya kifo, Gadner alijipatia umaarufu kutokana na aina ya utangazaji wake kupitia vipindi vya jioni ambapo alianzia katika kituo cha redio cha Clouds FM baadaye Times FM, E-FM na kisha kurejea Clouds FM.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags