Gamond bado hajaielewa nafasi ya mshambuliaji

Gamond bado hajaielewa nafasi ya mshambuliaji

Licha ya ‘klabu’ ya #Yanga kumsajili Hafiz Konkoni ambaye hadi sasa tayari amefunga mabao mawili kwenye kikosi hicho mapema msimu huu lakini bado inaonesha kiwango chake hakijakata kiu ya ‘kocha #Gamond.

Inadaiwa ‘timu’ hiyo bado inaendelea kutafuta mshambuliaji taratibu licha ya kuwa ni kweli ‘timu’ inashinda kwa mabao ya kutosha lakini ‘kocha’ huyo anataka ufanisi zaidi wa kutumia nafasi ambazo wanatengeneza pindi ‘timu’ inapo kuwa uwanjani.

Inaelezwa kuwa Gamond anataka mshambuliaji ambaye kwenye nafasi tatu atafunga mbili au zote anaona ‘timu’ inatengeneza nafasi zaidi ya ushindi ambao wanaupata.

Ingawa  kwa sasa ‘timu’ hiyo imefungiwa kusajili kutokana na kushindwa kumlipa stahiki yake, kiungo Gael Bigirimana. Mbali na kesi hiyo, pia Yanga inakabiliwa na mtihani mwingine baada ya ‘beki’, Mamadou Doumbia aliyekimbilia Fifa kushitaki kuvunjika kwa mkataba wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags