Gabo Zigamba atunukiwa tuzo ya heshima Iringa

Gabo Zigamba atunukiwa tuzo ya heshima Iringa

Mwigizaji Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ ametunukiwa tuzo ya heshima Mkoani Iringa kufuatia na ubunifu wake katika uigizaji.

Tuzo hizo za ‘Chama cha Waigizaji na Wacheza Filamu Tanzania (TDFAA)’ Mkoa wa Iringa zilizotolewa Agosti 05, 2024, wakati wa hafla hiyo mwigizaji huyo aliwataka wasanii wa Iringa kuongeza juhudi, ubunifu, na nidhamu katika kazi zao.

“Kwa msanii chipukizi yeyote maneno mazuri ambayo anatakiwa ayachukue kutoka kwangu au kwa mtu mwingine yeyote ni nidhamu, hakuna kitu kama nidhamu ingawa kila mtu ana tabia zake na ana namna ambavyo amelelewa lakini ukishakuwa na nidhamu basi kuna uwezekano kwa asilimia 98 ya kufanikiwa” amesema Gabo.

Aidha amewapongeza wasanii katika Mkoa wa Iringa kwa kazi nzuri wanayoifanya na kusema kuwa wanahitaji vitu vidogo vidogo vya kitaaluma ili kuwa bora zaidi huku akiwaomba wawekezaji kuwekeza kwa wasanii hao.

Gabo ametunukiwa tuzo hiyo kutokana na ubunifu wake ambao anauonesha kwenye tamthilia mbalimbali kwaongea kama wamakonde, wamasai na wapemba.

Wasanii wengine waliohudhuria katika utoaji wa tuzo hizo mkoani Iringa ni Lamata, Halima Yahya, Love Juakali, Bi staa na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags