G Son afariki dunia akiwa Marekani

G Son afariki dunia akiwa Marekani

Aliyekuwa rapa wa kundi la Xplastaz nchini, Godson Rutta G San (G Son) amefariki dunia akiwa nchini Marekani.

Taarifa zinasema G Son ambaye jina lake halisi ni Godson Rutta aliyekua Chicago,Illinois Marekani amefariki dunia siku ya jana Machi 23, 2025 nchini humo.

Rapa huyo alikua ni sehemu ya kundi lenye heshima katika Hiphop ndani na nje ya Tanzania kupitia kundi lao la Xplastaza tokea Arusha.

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na familia mipango ya mazishi inaendelea ili kuweza kumpumzisha katika nyumba yake ya milele G Son huko nyumbani kwao Arusha,Tanzania. Hata hivyo chanzo cha kifo chake bado hakijawekwa wazi

G SAN atakumbukwa kama rapa na MC wa kwanza wa Tanzania kushiriki katika moja ya Cypher ya international 'Bet Cypher' mnamo mwaka 2009 akiwa na wasanii wakubwa kama Nippsey Hussle, Wale na KRS One






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags