Freddy atoa ya moyoni baada ya kutemwa Simba

Freddy atoa ya moyoni baada ya kutemwa Simba

Saa chache baada ya kutemwa rasmi na Simba, mshambuliaji Freddy Michael Kouablan amevunja ukimya na kufunguka ya moyoni, akisema alichofanyiwa na mabosi wa klabu hiyo kwake imekuwa ni kama sapraizi kwani alikuwa amejipanga kufanya makubwa baada ya kujipata mwishoni mwa msimu uliopita.

Pia mshambuliaji huyo wa zamani wa Green Eagles ya Zambia, amesema licha ya kuwaheshimu na kuwakubali mastraika wapya waliotua Msimbazi, lakini amewaponda kwamba hakuna yeyote wa kumfikia kwa kazi ya kufunga, hata kama alianza na mguu mbaya aliposajiliwa katika dirisha dogo la msimu uliopita.

Freddy alitua Msimbazi katika dirisha hilo akitokea Zambia alipoacha akiwa na mabao 11 katika mechi 17 za Ligi Kuu ya nchi hiyo, mbali na mabao mengine matatu ya michuano mingine na akiwa Simba akiifungua mabao sita ya Ligi Kuu Bara, mawili ya Kombe la Shirikisho na moja la Kombe la Muungano.

Soma zaidi www.mwananchi.co.tz






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags