Fireboy dml aukosoa muziki wa Afrobeat

Fireboy dml aukosoa muziki wa Afrobeat

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Fireboy DML, ameukosa muziki wa #Afrobeat kwa kudai kuwa muziki huo hauna mtiririko mzuri wa uandishi baada yake unabebwa na ‘vaibu’.

#FireboyDML ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahojiano yake na Billboard News, ambapo aliweka wazi kuwa muziki huo umekuwa ukichezwa tuu kwenye ‘vilabu’ vya starehe kuliko kuibua hisia za watu wasikilizao muziki huo, huku akidai kuwa muziki huo umekosa uandishi mzuri, hauna mpangilio katika mashairi kinyume chake unabebwa na vibe tu.

Muziki wa #Afrobeat au kwa jina lingine ‘Afrofunk’ ni aina ya muziki wa Kinaigeria ambao unahusisha mchanganyiko wa mitindo ya muziki wa kitamaduni wa #Kiyoruba na #Igbo

Fireboy anatamba na vibao vyake kama ‘Vibration’, ‘Peru’ ‘Outside’, ‘YAWA’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags