Filamu ya George Floyd kutayarisha na mtoto wake

Filamu ya George Floyd kutayarisha na mtoto wake

Mke na mtoto wa marehemu George Floyd wameripotiwa kutayarisha filamu iitwayo ‘Daddy changed the World’ ya maisha ya mwanaume huyo ambaye aliuwawa na polisi nchini Marekani mwaka 2020.

Kwa mujibu wa tovuti ya Variety mke wa mwanaume huyo aitwaye Roxie Washington na binti yake Ginna Floyd watashirikiana na Gregory R. Anderson, ambaye ni mtayarishaji wa filamu ya ‘The Family Business’ katika kukamilisha mradi huo.

Ikumbukwe kuwa George Floyd (46) aliuwawa na Mei 20, 2020 na polisi wa Marekani Derek Chauvin kwa kumpigia magoti kwenye shingo zaidi ya dakika tisa na kupelekea kifo chake, Floyd alikamatwa na polisi huyo baada ya kudaiwa kujaribu kutumia noti bandia ya $20 kwenye duka.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags