Fei toto: Kisa yanga mpenzi wangu aliniacha

Fei toto: Kisa yanga mpenzi wangu aliniacha

Aliyekuwa mchezaji wa Yanga Fei Toto amefunguka makubwa na kueleza kuwa sakata lake na ‘klabu’ ya Yanga la kuvunja mkataba lilimfanya akaachana na mpenzi wake aliyempenda sana.

Fei Toto ambaye kwa sasa anakipiga katika ‘klabu’ yake ya Azam Fc ameeleza kwa undani baada ya kufanya mahojiano na gazeti la Mwanaspoti kwa na kusema kuwa…

“Lile sakata liliniathiri kwenye mambo mengi sana sio kwa upande wa kucheza pekee, wakati niko kwenye wakati mgumu kama ule kila wakati unafikiria hii kesi itaishaje, nikakutana na pigo lingine la kukimbiwa na mpenzi wangu ambaye niliamini ningekuja kumuoa.

Aliona kama maisha yangu ya soka tena basi ndio yameishia pale alishindwa kuvumilia na kuamua kutafuta mtu mwingine kitu kilichoniumiza zaidi ni hatua mbaya zaidi kwangu ikawa kwenda kuolewa tena nikiwa katikati ya lile sakata,

Sikuwa nimemuoa ila tulikuwa na mipango mingi ya maisha kati yetu, hakutaka kuvumilia kabisa nililazimika kuyapokea maamuzi yake hakukuwa na namna na sasa nimerudi uwanjani maisha mengine yataendelea tu.”
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags