Fei toto, Bangala, Aucho kuukosa  mchezo wa leo

Fei toto, Bangala, Aucho kuukosa mchezo wa leo

Vinara wa Ligi Kuu soka Tanzania bara Yanga SC itawakosa wachezaji takribani wa nne kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC unaochezwa leo Aprili 06, 2022 ndani ya dimba la Azam Complex Chamazi Jijini Da es salaam.

Taarifa kutoka kwa Kocha msaidi wa Yanga Cedric Kaze amethibitisha kuwa kuelekea mchezo dhidi ya Azam FC watawakosa wachezaji Feisal Salum ‘Fei Toto, Khalid Aucho kutokana na majeruhi lakini pia mchezaji Yannick Bangala Litombo aliumia juzi mazoezini watamuangalia kama ataweza kucheza  na Faridi Musa anaumwa.

Kocha kaze pia amesema wachezaji Crispin Ngushi, Abdallah Shaibu ‘Ninja, jesus Moloko wote  wanafanya mazoezi na timu pamoja na wachezaji wengine  baada ya kupona majeruhi na wataangalia kama watakuwa vizuri kuwa sehemu ya mchezo huo.

Kukosekana kwa Aucho, Bangala na Feisal kuna ifanya Yanga kusalia na vingo wa kati wawili tu ambao wapo fiti kucheza kesho ambao ni Zawadi Mauya na Salum Abubakari Sure Boy.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags