FARAJI: Kila mtu apiganie kipaji chake

FARAJI: Kila mtu apiganie kipaji chake

Muziki ni jambo ambalo linashabikiwa sana na vijana wengi licha ya kuwepo kwa wimbi kubwa la wasanii hapa kwetu bongo lakini bado underground wanafufuka kila inapoitwa leo.

Hapa kwenye muziki bhna tunazungumzia aina za uimbaji ikiwemo bongo flavour, RNB, Singeli, Hip Hop, Taarab na ladha nyengine nyingi.

Vijana mbalimbali wamekuwa wakipambana katika  Tasnia hii ya sanaa ili kuonyesha uwezo walionao, leo namleta kwako kijana maridadi kabisaa anaetambulika kwa jina la Faraji Hamis Nakopa maarufu Wizzle Nakopa.

Faraji ni Mwanafunzi kutoka Chuo kikuu cha SUA kilichopo mkoani Morogoro akiwa anachukua degree ya liboratory Science and laboratory Technology.

Akiwa mwaka wa pili Chuoni hapo kijana huyu ni anakipaji mashuhuri kabisa cha uiambaji wa muziki wa bongo flavour ambao ndiyo anaoukubali zaidi hapa nchini.

Akizungumza na mwandishi wa makala haya Faraji ameweka wazi kuwa yeye ni mtu ambaye anaikubali sana sanaa na anamalengo makubwa kupitia sanaa yake.

“Awali wakati naanza kuimba nilianza na nyimbo za Hip Hop lakini mapokeo yake hayakuwa mazuri kwa upande huo hivyo nikabadilisha gia angani nikaanza kupambana na bongo flavour hatimaye umenifikisha hapa nilipo sasa.”anasema

Uligundua vipi kipaji chako?

Akielezea namna alivyoanza kugundua kipaji chake hicho na kuvutiwa zaidi na  muziki huu wa kizazi kipya kijana huyu amesema kuwa Shule ndiyo iliyosababisha agundue uwezo na kipaji alichonacho.

“Nakumbuka wakati niko Sekondari nilikua Mwandishi wa Mashairi na  kuimba ngonjera kukiwa na matukio nilikua nafuatwa na walimu napewa kazi hiyo mashairi yaliwavutia sana wanafunzi wenzangu hivyo nikawa mtunzi mashuhuri shuleni hapo”anasema.

Wimbo wako wa kwanza ni upi?

Kichupa cha  kwanza alichokitoa kijana huyu  kilikwenda  kwa jina la ‘NAJUTA’ ambao aliimba kwa mfumo wa kufoka  wenyewe wanaita Hip Hop ambao kwa mujibu wake anasema mfumo huo haukupokelewa vizuri sana na mashabiki zake.

“kiukweli mapokezi kwenye Hip Hop hayakuwa mazuri ndipo nikaamua kujiongeza kwa kubadilisha dira na kuimba kwa mfumo wa bongo flavour na hatimaye matumaini makubwa nikapata kupitia aina hiyo ya uimbaji”anasema.

“Hivi tunavyozungumza hapa nimetoka kuachia Audio yangu pamoja na video kama wiki mbili zilizopita muamko nilioupata ni mkubwa sana kwa upande wangu kwasababu mimi ni underground hivyo naweza kusema kuwa nimeanza vizuri ” anasema.

Vile vile ameeleza kuwa kupitia wimbo alioutoa hivi karibuni unaokwenda kwa jina la ‘NITAKUSAU’ ndiyo wimbo unaofanya vizuri kwani umeibua kipaji chake na kufahamika zaidi kwa kadamnasi.

“Nashukuru kiukweli kwani hadi sasa audio ya wimbo huu ina viwers mia 400  lakini pia video inatakribani viwers 1000 ndani ya mwezi ni jambo kubwa kwangu”anasema.

Ndoto zako ni zipi kwenye tasnia hii?

Hata hivyo kijana huyu ameeleza ndoto zake kubwa kwenye tasnia hii ya muziki wa bongo flavour ni kuja kufanya kazi kwa  kushirikiana na makundi makubwa ya muziki hapa nchini ikiwemo Wasafi, konde gang, na kings music.

“lebo yoyote kati ya hizo nitakayobahatika kuingia itakua ni Baraka pia kwani itakua ni sehemu moja wapo ya kukuza na kuendeleza uwezo nilionao kwenye tasnia hii” anasema na kuongeza.

“Nafurahi pia Chuo ninachosoma kinanipa support hususani wanafunzi wenzangu wameonyesha namna wanavyokubali kazi zangu ambazo nazitoa “ anasema.

Licha ya faraji kujihusisha na masuala ya burudani lakini kijana huyu ni msomi mzuri kabisa anaechukua course ya library science and library technology akiwa na malengo madhubuti kwenye karia yake hiyo.

“Tangu niko Sekondari nilikua nasomea mchepuo huu wa Science nikiwa na malengo yangu binafsi katika hili ambalo nasomea kwasasa sio kwamba naimba ukafikiri mimi nitakua sina future hapana niko vizuri zaidi kwenye masomo pia”anasema.

Hata hivyo anasema kuwa yuko sehemu sahihi kwa course ambayo anaisomea na malengo yake ni kufanyia kazi kile ambacho anakisomea chuoni hapo.

“Nahitaji kufanya kazi kupitia course yangu hapo nitakua na furaha zaidi kuliko nitakapoenda tofauti  na nilichosomea lakini kikubwa kuangalia uwanja wa fursa pia namna zinavyopatikana.”

Hata hivyo amewashauri vijana wenzake na wanafunzi walioko vyuoni kuhakikisha wanatoka nje ya box kutazama mbali zaidi kwani wanatakiwa kuwa na vitu vya ziada na sio kutegemea masomo pekee kuwa yatawatoa kimaisha.

“Waangalia upande wa pili wa shilingi na  kupigania viapaji vyao kwani ni njia pekee ya wao kuwatoa kila mtu anauwezo aliobarikiwa na Mungu basi watumie fursa hii pia”anasema.

Changamoto anazokumbana nazo kimuziki

Hata hivyo anasema wazazi wake wamekua ndiyo support yake kubwa sana kwenye kazi zake licha ya kuwepo kwa uhaba wa kifedha katika kuendesha muziki wake.

“Kiukweli Changamoto kubwa ni masuala ya financing kwani kuendesha muziki kunahitaji pesa kutokana na video ambazo natakiwa kuzifanya kunagharama hapa kwa sisi underground unakuta video moja laki 500,000 hadi 60,0000 sasa ukiwa huna kipato huwezi kutoboa” anasema.

Namna anavyobalance muziki na masomo yake

“Binafsi yangu huwa najihusisha na muziki kipindi cha likizo yani mwishoni mwa semister na muda wa masomo unapowaidia huwa sijihusishi na masuala ya muziki nazingatia masomo kwanza”.

Je unawaeleza vipi wasanii chipukizi ambao wanataka  kujitumbukiza kwenye tansia kwa sasa?

“ Watambue kuwa muziki ni safari wasichukulie kama muziki ni tukio hapana  kwani unaweza kuimba hata miaka 4 bila mafanikio hivyo muziki hauna tofauti na masomo unavyoyaona” anasema na kusisitiza kuwa.

“Unaanza chini huku kisha unapanda ngazi za juu hivyo ndivyo maisha yamuziki ninavyoyafananisha na masomo hivyo wanatakiwa kutambua kuwa muziki ni process.”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post