Fanya hivi kupata simu yako iliyopotea

Fanya hivi kupata simu yako iliyopotea

Imekuwa kawaida baadhi ya watu, kusahau sehemu ambayo wameacha simu zao. Jambo hili huumiza kichwa zaidi ikiwa simu imewekwa ‘silent’,  kwani hata mmiliki akitaka kufahamu sehemu ilipo inakuwa ngumu

Ulimwengu wa teknolojia umerahisisha mambo, zipo njia za kuitafuta simu yako na ukaipata kirahisi hata kama imezimwa au imetolewa sauti.

Fanya haya kupata simu yako

1, Unachotakiwa kufanya fungua web browser kwa kutumia Laptop ‘PC’, kisha search Google.

2, Baada ya kuipata Google, nenda upande wake wa search andika maneno haya, ‘find my phone’ .

3, Kwa kufanya hivyo itakuletea machaguo, bonyeza maneno yenye rangi ya buluu yaliyoandikwa  ‘Find my Phone’

4, Ukibonyeza maneno hayo yatakupeleka moja kwa moja kwenye ramani inayoonesha simu yako ilipo, pia itakupa machaguo ya kuipiga simu yako au kuifunga.

5, Ili kuipiga simu yako bonyeza maneno yaliyoandikwa ‘play sound’ ukifanya hivyo simu yako itaanza kuita popote ilipo ndani ya dakika tano mfululizo, hata kama ikiwa silent. Hivyo kama ipo karibu utaiona

6, Chaguo jingine limeandikwa ‘Secure device’ hili litakusaidia kuifunga simu yako na kuondoa akaunti ya Google kwenye simu hiyo.

Kwa watumiaji wa simu za Iphoe pia wanaweza kupata simu zao kupitia iCloud.com., kwa kuandika neno ‘find my iphone’. Zingatia kutumia Laptop (PC) wakati unatafuta simu yako.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags