Fanya haya kuepuka uvivu kazini

Fanya haya kuepuka uvivu kazini

Mambo vipi, furaidayy ndo kama hiyo bwana I hope uko poa mwanetu sasa pamoja na weekend lakini hatuja poa kukujuza mambo mbalimbali yanayojiri  kitaani au sio sasa wiki iliopita katika segment ya kazi tulikujuza kuhusiana na njia za kumwambia bosi wako kuwa unatatizo namfanya kazi mwenza. Sasa kama bado hujaisoma fanya kupitia websit yetu ukajifunze Zaidi.

Leo tutazungumzika tabia ya uvivu kazi hii imezoeleka sana kazini tena hasa mfanyakazi anapoizoea kazi au ofisi Fulani anakuwa na tabia za kutotimiza majukumu yake, sasa leo tumekuja kuzungumza na nyie hatuwezi kuwakalia kimya nah ii yote ni kusaidiana kutokupoteza kazi yako.

Naenda kukusogeza baadhi ya mbinu ambazo ukizifanya utaepuka uvivu kazini…

  • ONGEZA UBUNIFU

Kufanya hivi kutakufanya usiwe mvivu kazini ukiwa mbunifu na ukatumia njia mpya kukamilisha majukumu yako ya kila siku hii ita kusaidia kila siku kuwa na kitu kipya katika akili yako hivyo hautaona uvivu kwakuwa akili yako itakuwa inawaza kuchakarika tuu muda wote.

Ili kufanikiwa lazima pia uweke au utengeneze mazingira ya kufanikiwa, ambapo ili uwe na uhakika wa kufanikiwa katika jambo unalolifanya inategemea misingi ambayo umejiwekea, ambayo ni kama ifuatayo tambua umuhimu na msaada wa imani katika kufanikiwa kwako.

  • EPUKA KUGHAIRISHA KAZI

Asilimia kubwa ya watu wanapenda kughairisha mambo haswa walioko maofisi, so usipendeleee kufanya jambo hili maana ndo mwanzo wa uvivu kama kazi umekuja ifanye hata kama ni ngumu ifanye kwa uchache harafu ukije kesho unamalizia palipo baki.

Epuka sana sana jambo hili litakusaidia kuondoa uvivu wote ulionao na sio hivyo tuu pia itakupunguzia kuwa na malimbikizi ya kazi yaani kuwa na kazi nyingi katika ofisi yako.

 

  • TENGENEZA USHIRIKIANO KAZINI

Kuwa na mtandao wenye ushirikiano mzuri wa kushare mawazo na marafiki wachapakazi itasaidia kupata mawazo mapya na itakupa hamasa ya kufanya kazi kuna msemo wanasema ukikaa na waridi lazima unukie mwanetu.

Sasa fanya urafiki na wafanyakazi walio mahodari wa kazi mimi nakwambia hauwezi kuwa mvivu.

  • ACHA KUISHI BILA MALENGO

Mafanikio sio kitu ambacho hua kinatokea kwa bahati mbaya ili kuwa na tumaini la mafanikio kupatikana lazima ujifunze kua na mipango madhubuti ya kufanikiwa na uthubutu mtiifu wa kuchukua hatua kadhaa kuelekea kijiji cha mafanikio, achana na tabia ya kufanya kazi tu bila kujua lini au saa ngapi utafanikiwa.

Malengo yatakufanya kilakitu kazini ufanye kwa wakati na hautakuwa na muda wakupoteza na siku zote ukijiwekea mpangilio katika maisha yako lazima utafanya kakwabidii zako zote ili ufanikishe jambo Fulani.

Ukiangalia kuna watu nyuma yako wanakutegemea au nakufanya wewe ni mfano kwao huwenda ikawa familia ndugu na jamaa lazima utaacha uvivu so jitambue mapema wewe ni nani.

  • PENDA UNACHOFANYA

Penda mipango yako penda kazi unayofanya ili kukuongezea msukumo wa ndani wa ufanyaji kazi itakusaidia kufanya kwa bidii bila kuchoka na muda wote utatamani uwe kazini

 Pia siku zote ukipenda unachokifanya lazima utakuwa nashauku kutaka kujua mambo anayo husu hicho kitu ususani kazi ukijiwekea utaratibu wakuipenda kazi yako na ukaikubali basi hauta hisi hali ya kuichoka kazi au kuidfanya kwa uvivu.

usikubali kurahisisha kazi et ukisema unafanya ilimradi tu umalize kwamba atajijua bosi na kampuni yake  ata kampuni ikishuka kiuwezo wewe haikuhusu wala hauna uchungu.

  • KUA NA RATIBA NA MIPANGO YA MAENDELEO

Hakikisha una ratiba ya kukuelekeza muda na ukomo wa kufanya mambo yako lakini pia mipango na madhubuti na mikakati makini itakayo kufanya ufikie mafanikio uyatakayo. Unahitaji ubunifu mkubwa katika kutimiza hatua hii, ili uweze kupanga mipango yenye kuendana na uwezo wako.

Heshimu ratiba na mipango uliyojiwekea kwa kuhakikisha unafanya kila ulichopanga kwa wakati na uamini kua maamuzi yako na unachokifanya ni sahihi, usifuate maneno au mawazo ya mtu mwingine kwa umbea hiyo itakusaidia kufanya kazi kwa bidii, akili na kwa nguvu zako zote.

Weka dhamira ya kweli kuhusu kufanikiwa na mafanikio yako, hakikisha unadhamiria kutoka moyoni kufanikiwa kwa namna au hali yoyote ile pendelea kufanya mazoezi epukaa muda mrefu kazini itakusaidia kutoona uvivu kazini.

Nasemajee!! Siku zote ni kheri ucheze na mshahara usichezee kazi mwanetu waulize wale wanetu walio chezea kazi watakwambia hali ya hewa ikoje mtaani bila kazi, amka sasa acha uvivu utakukosti baadae.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags