Fally Ipupa kufunguliwa mashitaka Uganda

Fally Ipupa kufunguliwa mashitaka Uganda

Kampuni ya 243 Events ya kutoka nchini Uganda imepanga kumfungulia mashtaka mwanamuziki kutoka nchini Congo Fally Ipupa kudai haki yao baada ya mwanamuziki huyo kushindwa kutokea kwenye show nchini humo mnamo mwaka 2019.

Inaelezwa kuwa kampuni hiyo ilishirikiana na uongozi wa #FallyIpupa, ukiongozwa na Madina Djoboungue wa Mad Mad Production, kwa ajili ya kuandaa tamasha lililokuwa limepangwa kufanyika Uganda mwaka huo.

Ambapo 243 Events wanadai walilipa pesa za awali Pauni 85K zaidi ya tsh 259 milioni  ili kuhakikisha wanampata msanii huyo, kisha wakaongeza Pauni 10K sawa na tsh 31 milioni , lakini bado show haikufanyika na pesa hazikurejeshwa.

Pamoja na kampuni hiyo ilijaribu kupata suluhu ya shutuma hizo, mchakato huo ulizuiwa na uongozi wa Fally Ipupa na kuwa wanaangalia njia ya kurudisha gharama walizomlipa msanii huyo na hakutokea kufanya show.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags