Fainali za NBA 2024 zaweka rekodi

Fainali za NBA 2024 zaweka rekodi

Fainali za mpira wa kikapo Marekani NBA zimeripotiwa kuweka rekodi mpya ya bei ghali za ‘tiketi’ tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011 ambapo kwa sasa ‘tiketi’ moja imefikia dola 4,150 sawa na Sh 10 milioni.

Bei hiyo inapita kiwango cha juu cha mwaka 2019 ambapo kilikuwa ni dola 3,899 huku umaarufu na ongezeko kubwa la mashabiki likitajwa kuwa chanzo cha ongezeko la bei ya ‘tiketi’ hizo.

Aidha kwa mujibu wa tovuti ya Wealth imeweka wazi kuwa ilifanya mahojiano na baadhi ya mashabiki wa mchezo huo ambapo walieleza kuwa kwao hawahofii ongezeko hilo la bei wapo tayari kutoa kiasi chochote kwa ajili ya kushuhudia fainali hizo moja kwa moja (live).

Utakumbuka kuwa bei za tiketi hizo kwa miaka ya nyuma zilikuwa dola 945 (2011), dola 853 (2012), dola 947 (2013), dola 837 (2014), dola 1,604 (2015), dola 1,931 (2016), dola 1,767 (2017), dola 1,467 (2018), dola 3,899 (2019), dola 2,747 (2021), dola 3,657 (2022), huku 2023 tiketi ikigharimu dola 2,349.

Fainali hizo zinatarajiwa kuchezwa Juni 23, 2024 huko Dallas ambapo ‘timu’ ya Dallas Mavericks itachuana na Boston Celtics kuwania kombe la Larry O'Brien.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post