Fahyma Aongeza Mahari yake

Fahyma Aongeza Mahari yake

Hii sasa kali, Mwanamitindo maarufu nchini Fahyma  au  Fahyvanny ambaye kwa mara nyingine ameibua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudai kwamba uzuri wake umeongezeka maradufu hivyo mahari imeongezeka kwa mwanaume yeyote mwenye mpango wa kumchumbia.



Fahyvanny ambaye wengi walimjua kutokana na kuchumbiana na msanii Rayvanny au Vanny Boy kiasi cha kutumia jina la msanii huyo na kuunda lake anasema kwamba uzuri wake kwa siku za hivi karibuni umezidi kunoga na bei ya mahari haitabaki palepale ilipokuwa kwani nayo lazima itaongezeka vilevile.


Fahyma anasema; “Nyie nyie, naomba mahari iongezeke, siyo kwa uzuri huu…” Wafuasi wanaomfuatilia kwenye mtandao wa Instagram walionekana kumjibu makali mubashara huku wengi wakionekana kumsema kwamba hana uzuri wowote bali ni vipodozi tu ndivyo vimechangia kwa asilimia kubwa ya uzuri wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags