Fahamu zaidi kuhusiana na uzazi wa mpango

Fahamu zaidi kuhusiana na uzazi wa mpango

Heeeey! I hope mko well, am here kuelekezana kuhusiana na maswala mazima ya Afya hususani ya wanawake, maana wengi wenu mnanitambua kama Madam hedhi salama, sasa leo katika topic yetu ya kwanza kabisa tutazungumzia jambo ambalo kwasasa linatrenda sana kupitia mitandao ya kijamii.

Kuhusiana na swala zima la wanawake wengi kutumia uzazi wa mpango, kuna baadhi ya watu wanatumia tuu hivi vitu bila ya kushauriwa na madaktari, leo nawafahamisha Zaidi kuhusiana na uzazi wa mpango.

Hakuna kitu kizuri sana duniani kama mtu kuwa na mtoto ni kitu kizuri sana ila ni muhimu mtoto huyo akija aje kwa wakati muafaka na sio surprise, ndio kuna surprise nzuri na mbaya lakini surprise ya kupata ujauzito huku una kitoto cha miezi 6 hiyo ni balaa na inamsababishia mtoto asikue vizuri kwani hukatishwa muda wa kunyonya kabla ya muda wake na mama hapati muda mzuri wa kupumzika baina ya mimba moja na nyengine.

Na hizi ndo njia za uzazi wa mpango…

Njia za uzazi wa mpango ziko za aina mbili:

1) Barrier mothed, hizi ni njia ambazo huzuia mbegu za kiume isikutane na yai kupevushwa mtoto...

Njia hizi ni kama...

  • Kumwaga Nje

Hii ni njia nzuri na isiyokua na madhara njia asilia ya kuzuia mimba ambayo haikuzuii kutofanya tendo la ndoa bali njia hii anaehusika asilimia kubwa ni mwanaume inampasa awe makini wakati wa kumwaga na badala yake amwage nje mwanaume anapojisahaua huwez kuplekea kupatikana kwa mimba.

  • Njia ya kalenda

Njia nzuri ya asili hutumii kemikali yoyote ilee inasaidia asilimia kubwa kujiepusha na kubeba ujauzito, shida ya njia hii inawataka wanandoa au wapenzi wakae zaidi ya siku 10 bila kufanya tendo la ndoa, zile za baada ya mwanamke kumaliza hedhi na siku za hatari.

2) Hormonal Method

Hizi ni njia ambazo zinazotumia kemikali kuzuia yai kutopevushwa au kuharibu mazingira ya yai kupevushwa.

Miongoni mwa njia hizi ni…

  • VIDONGE

Dawa za majira ambazo zinazozuia upatikanaji wa mimba, ni nzuri pia husaidia kuweka mzunguko wa hedhi sawa na kupunguza maumivu wakati wa hedhi, lakini inahitaji mtu sio msahaulifu kwani kusahau kumeza dawa siku moja tu huweza kusababisha upatikanaji wa mimba.

Kuna baadhi ya watu wanasema kuwa njia hii sio nzuri lakini kwa upande wangu mimi kama Nurse hii ni nzuri kuliko hata watu wanavyo izungumzia

  • SINDANO

Hii ndo njia nzuri zaidi kwasababu haihitaji mtu kukumbuka kumeza dawa kila dakika inakuweka huru na mtu anakua huru kufanya tendo la ndoa wakati wowote bila kuhofia siku za hatari.

  • KIPANDIKIZI

Hii ni njia ambayo kijiti kinawekwa chini ya mkono wa mwanamke kinasaidia kuzuia mimba kwa kuzuia yai lisipevushwe na ni njia ya muda mrefu vipo vya miaka 3 na mitano!! 

Hua vina maudhi madogo hueza kusababisha mwanamke kunenepa kidogo kuharibika kwa mzunguko ila ni maudhi madogomadogo ya mwanzo baadae huondoka.

Na hii ukiona inakukataa sana basi usijaribu kabisa kuweka maana inaweza kukuletea matatizo, kwasababu nishakutana na keshi nyingi mdada kashika mimba lakini yuko na kijiti hii inasababishwa na kijiti chenyewe kukukataa.

  • KITANZI

Hii nayo inafanya kazi kama kipandikizi imekaa na umbo la T ambayo inawekwa kweny tumbo la mimba ni njia ya uzazi wa mpango wa muda mrefu kuanzia miaka 10 hadi miaka 12.

  • KONDOMU

Hii ni njia ambayo watu wengi wanaijua lakini si wapenzi sana kuitumia ni nzuri husaidia kujikinga na maradhi pia ukiachana na mimba tu husaidia kujikinga na virusi vya VVU pamoja na Magonjwa mengine ya zinaa.

  • KUNYONYESHA BAADA YA KUJIFUNGUA MAMA ANAETOKA KUJIFUNGUA

Mama akinyonyesha ipasavyo (EBF : EXCLUSIVE BREAST FEEDING) yaani kumnyonyesha mtoto wa miezi 6 bila kumpa chochote kile   husaidia mama kutopata hedhi wakati wa miezi 6 na hii humuweka huru kutopata ujauzito na tafiti zimeonesha baadhi yao hawapati hedhi muda wa miaka miwili hadi pale wanapokatisha kunyonyesha.

Madhara ya utumiaji wa uzazi wa mpango…

Baadhi ya madhara yanatotajwa na wanawake wanaotumia uzazi wa mpango katika jumbe mbalimbali na ambazo baadhi yao yamethibitishwa kisayansi ni kama ifuatavyo;

  • Kupata ugumu wa kushika mimba.
  • Kutoka damu mara kwa mara.
  • Kuongezeka hamu ya kula.
  • Kupungua hamu ya kufanya tendo la ndoa.
  • Kuongezeka au kupungua mwili.
  • Kubadilika mzunguko wa hedhi.
  • Maumivu makali ya kichwa.

Tahadhari: sio kila njia ya uzazi wa mpango baasi ina madhara, cha kuwashauri kama unahitaji kutumia njia moja wapo basi fanya kumuona dactari anaehusika na maswala hayo kwa msaada Zaidi. Na ukitafuta tafuta docta ambae utakuwa unaenda kwake kama utapata changamoto yoyote kuhusiana na uzazi wa mpango utakao utumia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post