Fahamu upande sahihi wa kubebea pochi

Fahamu upande sahihi wa kubebea pochi

Tunakutana tena kwenye ulimwengu wa fashion ili kujuzana mitindo mbalimbali. Leo kwenye upande huu tutajuzana upande sahihi wa kubeba pochi.

Pochi ni moja kati ya kitu muhimu kwa wanawake ambacho hatakiwi kukikosa. Licha ya kuwa pochi humsaidia mwanamke kuhifadhi vitu vyake lakini pia huongeza umaridadi katika muonekano.

Mwanamke anayejipenda anapotoka kwenda sehemu lazima abebe pochi mkononi, lakini pia anashauriwa kubeba vitu vya msingi vinavyoendana na ukubwa wa pochi.

Pamoja na je umewahi kujiuliza ni upi mkono sahihi wa kubeba pochi au mkoba wako?

 

Magdalena John mkazi wa Kimara Bucha jijini Dar es Salaam amesema yeye hupendelea kubeba upande wa kushoto ili ule wa kulia aweze kufanya shughuli nyingine ikiwemo ununuzi wa bidhaa.

 

Kwa upande wake Nyasatu Robson anasema yeye hubeba mkoba wake katika mkono wowote na hana uelewa wowote juu ya mkono sahihi unaotakiwa kutumika kubebea pochi.

 

Kwa mujibu wa wataalamu na tovuti mbalimbali za masuala ya urembo na mitindo zinapendekeza mkoba kubebwa upande wa kushoto.

 

Kwa mujibu wa tovuti ya Afroswagga imeeleza kuwa pochi inatakiwa kubebwa upande wa kushoto ili kukupa urahisi katika kusalimiana na wengine kwa kutumia mkono wa kulia.

 

Pia inaelezwa kuwa kwenye manunuzi inakupa urahisi katika kuchagua vitu na kulipia manunuzi yako.

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                Unapobeba pochi kubwa na ile ya size ya kati kwa mtindo wa kuning’iniza katika maungio ya mkono inashauriwa kubeba vitu vichache kama unatamani kubeba pochi kwa mtindo huo.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                             

 

Pia inapendeza zaidi kwa pochi ndogo au za size ya kati zenye mikanda mirefu kuning’iniza katika biga lako kwani itakupa urahisi hata wakati wa kutembea.

 

Aina za pochi

Kwa mujibu wa mmoja wa wauzaji wa mapochi kwa njia ya mtandao, Shadiya Omari amesema kuna aina tofauti tofauti za pochi na huvaliwa kulingana na mtoko wa mtu husika.

 

Shadiya anasema pochi kubwa mara nyingi hupendelewa kubebwa na wanawake wenye watoto wadogo kwa ajili ya kubebea mahitaji mbalimbali au wajawazito na pochi za size ya kati ambazo wanawake wengi wanazo na huzibeba katika shughuli zao za kila siku.

 

Pia anasema kuna wallet na pochi ndogo ya mkononi (Clutch) ambazo hufaa zaidi kuvaliwa pindi mtu anapotaka kutoka akiwa amebeba vitu vichache vinavyobebeka kwa urahisi.

 

“Katika wallet unaweza kubeba fedha, vitambulisho, risiti na simu pia haipendezi kujazwa vitu hata ukashindwa kuifunga vizuri na Clutch ambayo watu wengi wanaita pochi hupendeza kuvaliwa unapokwenda katika sherehe au matembezi ya usiku na hutumiwa kubeba vitu vidogo ambavyo ni muhimu kuwanavyo unapokwenda shughulini kama fedha, kadi ya benki, simu au lipstick na wanya uliofungwa vizuri,” anasema.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags