Fahamu sababu keyboard kuchanganya herufi

Fahamu sababu keyboard kuchanganya herufi

Kwa kawaida kicharazio maarufu ‘keyboard’ za simu janja ama kompyuta huwa na mpangilio usiofuata mtiririko, yaani haianzii A-Z badala yake herufi zimechanganyika.

Kwa haraka unaweza kufikiri mtiririko huo upo kimakosa, lakini ukweli ni kwamba njia hiyo ya upangiliaji wa maneno iitwayo "QWERTY" ilibuniwa mwaka 1870 na Christopher Sholes ambaye ni mwanzilishi wa mashine ya kuandikia ya kwanza duniani.

Inaelezwa kuwa awali mashine za kuandikia zilikuwa zimepangwa maneno kwa mtiririko 'A-Z', lakini Christopher alibadilisha na kubuni iliyochanganya herufi kwa lengo la kupunguza kasi ya uandishi.

Sababu kubwa ya kufanya hivyo ilitokana na mashine za kuandikia kipindi hicho zilikuwa na tabia kuchelewesha, na kukwamisha baadhi ya meneno endapo mtumiaji ataandika kwa haraka.

Hivyo Christopher akaamua kuchanganya herufi ili kupunguza kasi ya kuandika wakati mtumiaji akiwa anatafuta herufi.

Lakini hata baada ya kukua kwa teknolojia kampuni mbalimbali za kompyuta na simu bado ziliendelea kutumia mfumo huo wa kuchanganya herufi. Mbali na zilizopo kwenye mfumo wa QWERTY pia kuna AZERTY na QZERTY.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post