Fahamu njia rahisi ya kupata passward za mitandao ulizosahau

Fahamu njia rahisi ya kupata passward za mitandao ulizosahau

Watu wengi wamekuwa wakipata changamoto ya kutokumbuka passward (nywila) zao za mitandao ya kijamii au application mbalimbali wanazotumia, wengi changamoto hiyo huwasababishia kufuta account zao ama kuzipoteza kabisa.

Leo kupitia Teknolojia tumekuletetea njia rahisi ya kupata passward zako zote ulizowahi kuzitumia kwenye kifaa chako cha kielektroniki.

Chakufanya

1, Hakikisha kwanza kwenye simu yako au kompyuta una akaunti ya google na unatumia browser ya Google Chrome

2, Fungua google chrome, kisha nenda mpaka kwenye upande wa kulia kwenye vidoti vitatu ambavyo ni option viguse, kisha bonyeza neno settings, chagua neno'Google Password Manager'

3,Bonyeza neno hilo 'Google Password Manager' ukifanya hivyo itakupeleka moja kwa moja kwenye kurasa ambayo utakuwa na uwezo wa kuona list ya mitandao na application ambazo umewahi kutumia na unazotumia sasa.

4, Ili uweze kuona password zako bonyeza unachokitaka kwenye list kisha utatakiwa kuweka fingerprint ama password yako ya simu au ya kompyuta na hapo utaweza kuona nywila uliyokuwa umesahau.

5,Lakini pia ndani ya hiyo page, utapata nafasi ya kuona password zako ambazo zinatajwa kuwa hatarini au zimevuja katika baadhi ya maeneo, kwa hiyo google itakushauri pia kuzibadilisha na kutengeneza password ambazo zenye ulinzi zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post