Fahamu madhara ya Human Hair

Fahamu madhara ya Human Hair

Na Glorian Sulle

Ni dhahiri kuwa suala la kuvaa na kubandika nywele /human hair kwa sasa ndilo linachukua nafasi kwenye ulimwengu wa fashion na mitindo. Ni muhimu kujali mwonekano wako, hasa linapokuja suala la nywele, kwani ndiyo hubeba haiba nzima ya mwanamke anapoenda sehemu yoyote.

Mbali na mwonekano bomba unaoweza kuupata endapo utavaa nywele hizo unapaswa kutambua madhara unayoweza kuyapata kutokana na kuvaa nywele hizo kama mtaalamu wa nywele Rose Oscar anavyoieleza Mwananchi Scoop.

Maambukizi ya ngozi, tukumbuke aina hii ya nywele, tunaita human hair ambapo asilimia 100% ni nywele za binadamu ni hakika binadamu huyu ana mengi kiafya kama ilivyo kwa binadamu yeyote yule, ikiwa nywele hazijaoshwa na kuandaliwa vizuri zinaweza kuleta madhara .

Rose anasema, kuna watu wanamzio (Allergies) na nywele au gundi inayotumika kubandika wigi hizo, kutokana na aina ya viatilifu vilivyotumika kutengeneza huenda zikawa na athari kwa aina fulani ya ngozi.

 

Anasema, aina hii ya mzio uharibu ngozi ya mtumiaji na  kuwa chanzo cha vipele au kuleta alama nyeusi na pengine kuwashwa na hatimaye ngozi kukosa mvuto.

 

“Uharibifu wa ngozi ya kichwa, hutokana na kukaa muda mrefu na  nywele na hata kusababisha ngozi ya kichwa kukosa nuru, kuuma, kupauka na hata kupukutika kwa nywele” amesema Rose.

 

Anaeleza kuwa, kutokana na ujazo wa nywele kichwani na kufunika kichwa muda wote kwa wale wenye ngozi maridadi (delicate) huishia kupata mba na miwasho kwa muda wote.

Maumivu ni moja ya madhara ya aina hii ya nywele. Kuna baadhi ya watu ubandikaji wao wa nywele hukaza mno yaani huvuta ngozi na kuibandikia wigi hali hii husababisha maumivu ya hali ya juu kwa anayebandikwa  na kumnyima uhuru.

“Kubandika nywele kwa nguvu sana au kwa kutumia gundi (glue) au bidhaa nyingine zenye kemikali zinaweza kusababisha maumivu ya kichwa au madhara mengineyo” ameeleza

 

Hata hivyo mabadiliko mengine yanayotajwa ni ukavu, ngozi kuwa nyeusi  na hata utango utango.

Nywele kunyonyoka kutokana na gundi zinazotumika kubandikia wigi kichwani kuwa na kemikali zake basi wakati wa kubandua wigi, hubanduka na nywele zako za asili na hata kukufanya kuwa na kipara, swala hili ni kwa wale wasiotumia kofia kubandikia wigi hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags