Fahamu mabwawa yanayowekwa pombe badala ya maji, Watu huogelea

Fahamu mabwawa yanayowekwa pombe badala ya maji, Watu huogelea

Starehe ni nyingi duniani na kila mmoja huwa na yake aipendayo, si ajabu starehe ya mtu mwingine ikawa kero kwako kwani watu hutofautiana katika machaguo.

Wapo wale wanaopenda kuogelea na mara nyingi huwakuta ufukweni au kwenye mabwawa maalum ya kuogelea (Swimming pools).

Wakati watu wengine wakitenga muda wao kwenda kwenye sehemu zenye maji ya kuogelea fahamu kuwa Austria ndiyo sehemu pekee duniani yenye bwawa maalum la pombe la kuogelea (Swimming pool ya pombe).

Imekaa kama simulizi ya kushangaza lakini ni uhalisia uliyopo Austria ambapo kuna mabwawa pekee ya kwanza duniani ya kuogelea yanayojazwa pint 42000 za ‘bia’ yanafahamika kama Schloss Starkenberger.

Licha ya mabwawa hayo kujazwa ‘bia’ lakini waogeleaji hawaruhusiwi kunywa ‘bia’ za kwenye mabwawa hayo kuokana na usalama wa afya zao kwani kila mtu huingiza mwili wake humo hivyo basi kwa mteja atakayetaka kulewa huruhusiwa kuchagua aina moja ya pombe kati ya 13 ilizopo kwenye orodha ya vinywaji na kisa hupatiwa kwa ajili ya kuburudika huku akiogelea.

Mabwawa hayo yana urefu wa futi 13 na hujazwa pinti 42,000 za ‘bia’, mtu anayetaka kuogelea kwenye pombe hizo hutakiwa kulipa dola 250 ambazo ni zaidi ya tsh 600k  kwa saa mbili.

Wateja wengi hupendelea kuogelea kwenye mabwawa  hayo kutokana na kupenda hali ya kunata na harufu ya pombe hizo lakini pia inasemekana husaidika kama matibabu ya mwili kuufanya uchangamke.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post