Fahamu kumbi 10 zenye uwezo wa kuingiza watu wengi

Fahamu kumbi 10 zenye uwezo wa kuingiza watu wengi

Mwananchi scoop ndo sehemu pekee tunayokukusanyia na kukuletea habari zote zinazohusu afya, mahusiano, michongo ya biashara na burudani. Basi bhana baada ya wasanii mbalimbali kuvunja record na hata kuingia kwenye orodha ya wasanii waliowahi kujaza kumbi za muziki.

Aidha watu wengi wanafahamu kumbi mbili maarufu duniani ambazo ni 02 Arena uliopo London nchini Uingereza na ukumbi wa Accor uliopo Paris na kuhisi ndio kumbi kubwa zaidi duniani zinazotumika kufanyia matamasha na matukio makubwa zaidi duniani.

Basi leo na kufahamisha kumbi 10 kubwa duniani ambazo ni;-

1. KJC King Dome unaingiza watu 75,000 uliopo Davao nchini Philippines
2. Philippine Arena unaingiza watu 55,000 uliopo Bocaue nchini Philippines
3. Saitama Super Arena unaingiza watu 36,500 upo Saitama nchini Japan
 4. Smart Araneta Coliseum unaingiza watu 30,000 upo Quezon nchini Philippines
5. SM Mall of Asia Arena unaingiza watu 27,500 upo Pasay nchini Philippines
 6. Baku Crystal Hall unaingiza watu 27,000 upo Baku nchini Azerbaijan
7. Mineirinho una uwezo wa kubeba watu 25,000 upo Belo Horizonte nchini Brazil
8. Arena Ciudad de México unachukua watu 25,000 upo Mexico City nchini Mexico
9. Štark Arena unachukua watu 24,300 upo Belgrade nchini Serbia
10. Greensboro Coliseum unachukua watu 23,500 upo Greensboro, North Carolina  nchini Marekani.

Vilevile  kumbi ndogo sana duniani ni ukumbi wa Accor uliopo Paris nchini Ufaransa una uwezo wa kuingiza watu 20,300, unachukua nafasi ya 37 duniani na ukumbi wa 02 Arena uliopo London Uingereza wenye uwezo wa kuingiza watu 20,000 na kuchukua nafasi ya 41 duniani.

Aiseeee! Katika kumbi hizo ni mara chache sana kusikia wasanii wa Afrika kujaza hizo kumbi, wasanii wenye uwezo kuzijaza kumbi hizo waliofanya mara nyingi ni marehemu Michael Jackson na baadhi ya wasanii wakubwa kutoka Marekani pia katika kumbi hizo hutumika kufanyia matamasha ya michezo mbalimbali ya Indoor kama basketball.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post