Fahamu kuhusu kukoma hedhi

Fahamu kuhusu kukoma hedhi

Mark Lewis

Mambo vipi watu wangu wa nguvu, kama kawaida yetu katika segment yetu ya afya tunaendelea kukujuza kuhusu maswala mbalimbali ambayo unayajua lakini tunakujuza zaidi, sasa leo tumekuja na swala zima la kukoma hedhi kwa wanawake.

Kukoma hedhi ni hali ya kawaida ambayo wanawake wote huipitia umri ukiwa mkubwa. Neno kukoma hedhi linaweza likaelezea mabadiliko yoyote yanayomtokea mwanamke muda mfupi kabla au baada ya kuacha kupata siku zake, ikiwa ni ishara ya mwisho wa kuzaa.

NINI KINASABABISHA KUKOMA HEDHI?

Mwanamke huzaliwa akiwa na idadi kamili ya mayai, ambayo hutunzwa ndani ya ovari. Ovari hizi pia hutengeneza homoni za estrogen na progesterone ambazo husimamia hedhi na upevushwaji wa mayai. Kukoma hedhi maana yake ovari kukoma kuachia yai kila mwezi na kusimama kuingia mwezini.

Kukoma hedhi ni sehemu ya kawaida ya mwili kuzeeka na hutokea baada ya kufikia umri wa miaka 40. Lakini baadhi ya wanawake wanaweza kukoma hedhi mapema zaidi, ikiwa ni matokeo ya upasuaji, kama hysterectomy au uharibifu kwenye ovari, kama baada ya tiba ya chemotherapy. Kukoma hedhi kabla ya miaka 40, kwa sababu yoyote ile huitwa premature menopause.

KUKOMA HEDHI MAPEMA

Kukoma hedhi kwa kawaida huwaje?

Kukoma hedhi kwa kawaida hakusababishwi na upasuaji au madawa. Ni mabadiliko ya taratibu yaliyo kwenye hatua tatu:

 . Perimenopause. Hatua hii huanza miaka michache kabla ya kukoma hedhi (menopause) wakati ovari taratibu zinaanza kupunguza utengenezaji wa estrogen. Kipindi hiki huenda hadi unapokoma hedhi, pale ovari zinapokoma kuachia mayai. Katika mwaka 1 au 2 kabla ya kukoma hedhi, utengenezaji wa estrogen hupungua kwa kasi. Ni katika kipindi hiki, wanawake wengi huona dalili za kukoma hedhi.

. Menopause. Hapa ni wakati mwanamke anapoona kuwa umepita mwaka mmoja tangu alipopata hedhi ya mwisho. Sasa ovari zilishaacha kutoa mayai na kutengeneza estrogen.

. Postmenopause. Hatua hii ni miaka ya baada ya kukoma hedhi. Katika kipindi hiki, dalili za kukoma hedhi kama hot flashes hupungua kwa wanawake walio wengi. Lakini madhara ya kiafya yatokanayo na ukosefu wa estrogen huongezeka kadiri umri wa mwanamke unavyoongezeka.

 Ni hali gani husababisha kukoma hedhi mapema

Kukoma hedhi mapema (premature menopause) kunaweza kusababishwa na;

. Urithi

. Matatizo ya kinga za mwili (autoimmune disorders)

. Kutokana na tiba za afya.

MADHARA YA KUKOMA HEDHI

. Premature ovarian failure. Kwa kawaida, ovari hutengeneza vyote, estrogen na progesterone. Mabadiliko katika viwango vya homoni hizi mbili hutokea, kwa sababu zisizoeleweka, na kusababisha mayai kusimama kutengenezwa mapema. Hali hii ikitokea kwa mwanamke aliye chini ya 40, huitwa premature ovarian failure. Tofauti na premature menopause, premature ovarian failure si lazima iwe ya kudumu.

. Induced menopause. Hii hutokea pale ovari zinapoondolewa kwa upasuaji kwa sababu za kiafya, kama uterine cancer au endometriosis. Induced menopause huweza pia kutokea baada ya uharibifu wa ovari kwa tiba za mionzi au chemotherapy.

 

DALILI ZA KUKOMA HEDHI

Wanawake wengi wanaokaribia kukoma hedhi wanapata hot flashes, yaani ghafla kusikia joto linalosambaa sehemu ya juu ya mwili, vikiambatana na hali ya kutahayari na kutokwa jasho. Hali hii huwa si kali sana kwa wanawake wengi lakini kwa wengine huwa mbaya.

Dalili nyingine zinazotokea mwanamke anapokaribia kukoma hedhi ni pamoja na;

. Hedhi zisizo na mpangilio au zinazorukaruka

. Kukosa usingizi

. Kusikia hasira mara kwa mara

. Uchovu

. Mfadhaiko

. Moyo kwenda mbio

. Maumivu ya kichwa

. Maumivu ya joints na misuli

. Mabadiliko katika kusikia hamu ya tendo la ndoa

. Uyabisi wa uke

. Shida kudhibiti haja ndogo

NB: Si wanawake wote wanaopata dalili hizi zote.

Matatizo ya muda mrefu yanayotokana na kukoma hedhi

Kukosekana kwa estrogen ndani ya damu kunakotokana na kukoma hedhi kumethibitika kusababisha baadhi ya matatizo ya kiafya yanayowapata wanawake wanapokuwa na umri mkubwa kukoma hedhi sababu wanawake waliokoma hedhi wanaweza kutokewa na yafuatayo:

. Mifupa kuwa nyepesi

. Magonjwa ya moyo

. Kibofu cha mkojo kutofanya vizuri na matatizo ya haja kubwa

. Hatari ya kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu

. Mikunyanzi ya ngozi

. Kukosa nguvu za mikono

. Kupungua kwa nguvu ya kuona 

Hata hivyo, hali hii ya kukoma kwa hedhi hutokea kwa kila mwanamke akishafika umri fulani, hivyo ni vizuri kwa mwanamke kujiandaa kukabiliana na hali hii pale inapokaribia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags