Fahamu kazi ya mistari iliyopo kwenye pini za earphone

Fahamu kazi ya mistari iliyopo kwenye pini za earphone

Imekuwa jambo la kawaida kukutana na mtu akiwa amevaa earphone masikioni mwake kwa ajili ya kuzuia sauti anayosikiliza isisikiwe na wengine. Lakini wakati wa ununuzi wa vifaa hivi wengi huzingatia zaidi muonekano wake, na sauti inayotoka bila kufahamu kuwa ni vyema, kuzingatia na kukagua mistari iliyopo kwenye pini za earphone au headphone.

Kama umewahi kuwa mfuatiliaji utakuwa umegundua kuwa pini za eaphone, headphone huwa na mistari na kawaida mistari hiyo hutofautiana, zipo zenye mmoja, miwili, mitatu na hata minne, na kila mstari huwa na kazi yake, kama ifuatavyo.

TRS Jack, hii ni pini yenye mistari mitatu (Tip, Ring, Sleeve) ambapo mstari wa juu kabisa huitwa 'Tip' kazi yake ni kupeleka sauti kwenye chaneli ya kushoto ya earphone, mstari unaofuata huitwa 'Ring', kupeleka sauti chaneli ya kulia na mstari wa mwisho 'Sleeve' husaidia kubalansi sauti ifikapo masikioni mwa msikilizaji na kuifanya isikike vizuri.

TRRS Jack, hii ni pini yenye mistari minne (Tip, Ring, Ring, Sleeve) pini za aina hii mara nyingi hupatikana kwenye headphone na kwenye vipaza sauti vyenye sehemu za kuchomekwa pini. Mstari wa juu 'Tip' kazi yake ni kupeleka sauti kwenye chaneli ya kushoto, mstari unaofuata 'Ring' ya kwanza hupeleka sauti chaneli ya kulia, 'Ring' ya pili ni kwa ajili ya kipaza sauti na mstari wa tatu 'Sleeve' husaidia kubalansi sauti inayotoka. TRRS huruhusu sauti pande zote mbili kwenye sikio la kulia na kushoto. Mara nyingi hutumiwa kwenye simu za mkononi, na laptop.

TS Jack, ni pini yenye mistari miwili (Tip, Sleeve) sauti inayosikika kwenye earphone yenye muundo huu hutoa sauti kwenye sikio moja, mstari wa juu 'Tip' hutoa sauti hupeleka kwenye chaneli ya kushoto na 'Sleeve' husaidia kuibalansi sauti isikike vizuri. Pini zenye TS mara nyingi hutumiwa kwenye gitaa la umeme, ambapo channel moja ya sauti inahitajika.

'Balanced Jack', hii huwa na mistari mitatu na mara nyingi hutumiwa kwenye headphone, husaidia sana kwenye kupunguza kelele, mistari hiyo mitatu husaidia kwenye kupeleka sauti chaneli ya kulia na kushoto pia kubalansi sauti.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags