Fahamu jamii ya watu wenye vidole viwili vya miguu

Fahamu jamii ya watu wenye vidole viwili vya miguu

Wahenga mwalisema kabla hujafa hujaumbika, na inafahamika kuwa si vyema kuwatenga watu kutokana na tofauti zao za kimaumbile. Imezoeleka kwenye jamii kumekuwa na watu wenye makabila mbalimbali ambayo huwa na sifa zake.

Sifa hizo wakati mwingine hutumika kama kitambulisho cha kabila husika, wakati wewe ukijisifia kuwa kabila lenu ni watafutaji wa pesa au mnaupendo basi fahamu kuwa kuna watu wanajivunia kuwa kabila lao linaasili ya watu wenye vidole viwili tu vya miguu ambavyo huviita miguu ya Mbuni.

Jamii ya watu wenye vidole viwili linafahamika kama Vidoma, hupatikana nchini Zimbabwe na uishi kando ya mto Zambezi, huzungumza lugha ya Dema, na hujihusisha hasa na uwindaji na ukusanyaji wa maunda.

Ingawa sayansi inaeleza kuwa na vidole viwili ni ulemavu ambao hutokana na matatizo ya mabadiliko ya chromosome, kitaalamu huitwa 'Lobster Claw Syndrome', hurithishwa kutoka kizazi moja hadi kingine, lakini kwa jamii iyo hawachukulii kama ulemavu bali huamini vidole hivyo ni baraka na hujisifia miguu ya aina hiyo huwasaidia kupanda miti kwa haraka.

Jamii ya watu hawa wanaustadi wa kutosha katika kutumia vidole vya miguu yao bila shida yoyote, hulazimika kuoa jamii ya aina yao, ndiyo maana jamii yao haisambai kwa watu wa makabila mengine.

Pia watu hawa huamini kuwa asili yao wametokea kwenye miti mikubwa aina ya mibuyu ambayo babu zao walidondoka kutoka juu ya miti hiyo na ndipo jamii ya watu hao ikaanza kuwepo duniani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post