Fahamu aina 5 ya Mazoezi hatari

Fahamu aina 5 ya Mazoezi hatari

 

 

Karibu msomaji wetu wa magazine ya Mwananchiscoop na leo katika kipengele hiki cha fitness tutaangalia aina tano ya mazoezi ambayo ni hatari na yanaweza kukusababishia majeraha.

Aina hizo za mazoezi ni kama yafuatayo

  1. Bicycle crunches

Ni mazoezi yanayoonekana rahisi ukimuona mtu akiyafanya kwani ni kama kuendesha baiskeli .lakini matatizo mengi hutokea wakati unapoibana vibaya misuli yako ya miguu unapotumia kasi kupindukia.

Pana hata uwezekano wa kukatika kwa baadhi ya misuli ya sehemu ya chini ya miguu na uchungu magotini .Endapo hujakuwa ukifanya mazoezi ya kujipasha misuli moto au umesusa mazoezi kwa muda mrefu, mazoezi aina hii si ya kurukia siku ya kwanza kabla ya mwili kuwa na uwezo wa kuyastahimili.

Wataalam wanashauri uyaanze pole pole na kuzidisha kasi yako pindi mwili wako unapoyazoea.

 

  1. Lat pull-downs (nyuma ya kichwa)

Ikiwa hutambui nafasi hatarishi unazoweka mwili wako, hutaweza kuzuia majeraha.

"Mazoezi haya yanaweka mkazo mwingi kwenye kapsuli ya pamoja ya bega na hatimaye inaweza kusababisha msukumo au hata kuraruka kwa baadhi ya sehemu za ndani za misuli ya bega " anasema Jessica Malpelli, DPT. Yeye ni tabibu katika Taasisi ya Mifupa ya Florida.

 

  1. The kettlebell swing

Umeziona kengele hizo kubwa zikibebwa na kurushwa na watu kwa uarahisi katika video. Kisha ukajishauri kwamba ni mazoezi unayoweza kuyafanya, umekosea kwa sababu hii ni mojawapo ya aina hatari Zaidi ya mazoezi .

Ingawaje yakifanywa vizuri na ifaavyo ni mazoezi bora ya kujipa nguvu, yanahitaji ufahamu wa mtindo unaotumia .

Wengi hufikiri kwamba mazoezi haya hutumia nguvu nyingi za mkononi lakioni ukweli ni kwamba nguvu za kuzungusha kifaa hiki zinatoka katika sehemu ya chini ya tumbo . ni vyema kujifunza njia bora ya kufanya aina hii ya mazoezi bila kujiumiza .

  1. Bent over rows

Mazoezi haya huhusisha kujipinda kwa kila sehemu ya mwili na wakati mwingine usipokuwa mwangalifu unaweza kujiumiza bila kufahamu hadi baadaye wakati uchungu unapozidi.

Wataalam wanashauri kufanya mazoezi haya wakati unapojipinda kuanzia kiunoni na wala sio upande sehemu ya upande mmoja hasa kama hujayazoea.

Wanaofanya vibaya mazoezi haya hujipata na majeraha mabaya ya uti wa mgongo au hata kukatika kwa mifupa inayounganisha misulu ya mgongoni na sehemu nyingine za mwili. 

Unaweza kujaribu kuyafanya kwa kutumia mpira maalum unaokuruhusu kujipinda bila kuwa katika hatari ya kuanguka.

  1. The Romanian dead lift

Ikiwa imefanywa kwa usahihi, ni mazoezi mazuri kwa mgongo na nyonga. Hata hivyo, ni mojawapo ya njia rahisi zaidi za kuumiza mgongo wako ikiwa hujui unachofanya. Kwa nini?

Wanyanyuaji wengi huzungusha migongo yao wakati wa kuinua au kuweka chini chumba kinachobeba uzani - na mara nyingi wanaweza hata wasitambue kwamba wanachofanya ni hatari .






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags