Esma: Hii ndio ndoa yangu ya mwisho

Esma: Hii ndio ndoa yangu ya mwisho


Baada ya kufunga ndoa usiku wa kuamkia leo na mpenzi wake Jembe One, mfanyabiashara na dada wa mwanamuziki Diamond, Esma Platnumz ameeleza kuwa ndoa hiyo ndio itakuwa ndoa yake ya mwisho.

Esma ameyasema hayo kupitia mahojiano yake na moja ya chombo cha habari ambapo ameeleza kuwa ndoa hiyo aliyoifunga jana itakuwa ndoa yake ya mwisho, vilevile Jembe ndiyo mwanaume atakeyezikwa naye.

Aidha ameweka wazi kuwa yeye na mumewe wameapia katika vitabu vya dini kwamba hawato achana.

Hii itakuwa ndoa ya tatu kwa Esma kwani alishawahi kufunga ndoa na Petit Man Wakuache mwaka 2014 ambapo walibahatika kupata mtoto wa kike aitwaye Taraji, pia mwaka 2020 alifunga ndoa nyingine ya pili na mfanyabiashara Msizwa, kwa upande wa Jembe aliweka wazi kuwa ndoa hiyo ndiyo ndoa yake ya pili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags