Eric ataka kulipwa zaidi ya 85 milioni ili aoneshe sura ya mtoto wake

Eric ataka kulipwa zaidi ya 85 milioni ili aoneshe sura ya mtoto wake

Kama ilivyo kawaida kwa baadhi ya watu maarufu kuficha sura za watoto wao mara baada ya kuzaliwa, kama ilivyojitokeza kwa baadhi ya wasanii na waigizaji nchini, mchekeshaji kutoka Kenya #Eric Omondi, naye ameungana na wanaoficha sura za watoto wao huku akidai kuwa ili aweze kuoneshe mtoto wake anatakiwa kulipwa Ksh 5 milioni.

Eric ambaye kwa sasa mpenzi wake ni mjauzito na anadai kuwa mwanamke huyo anatarajia kujifungua mtoto wa kike, amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na vyombo vya habari nchini humo, ndipo akatangaza dau hilo la Ksh 5 milioni ambazo ni zaidi ya Tsh 85 milioni.

Kutokana na kauli hiyo imewafanya baadhi ya mashabiki wake kumtolea maneno huku wengine wakidai kuwa anataka kumfanya mtoto huyo kama kivutio cha utalii kabla hata ajazaliwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags