Eric akubali kuonesha sura ya mwanaye baada ya kulipwa zaidi ya tsh 80 milioni

Eric akubali kuonesha sura ya mwanaye baada ya kulipwa zaidi ya tsh 80 milioni

Mchekeshaji kutoka nchini Kenya Eric Omondi amedai kuwa anatarajia kufichua sure ya mtoto wa kike aitwaye Kyla baada ya kulipa zaidi ya tsh 81 milioni kwa ajili ya kuonesha sura ya mtoto huyo. Eric anatarajia kufichua sura ya mtoto huyo Alhamisi hii, na anadai kuwa kuna mtu amelipa pesa kwa ajili ya kuionesha sura ya mwanaye. Awali Eric alisema kuwa hatokuja kunesha sura ya mwanaye hadi mtu alipe ksh 50 milioni, ambapo atakayelipa pesa hiyo ndiye atakuwa mtu wa kwanza kumuona mtoto na atapata nafasi ya kuitumika picha ya sura ya kichanga huyo katika biashara zake kama vile majariba ya watoto au maduka makubwa ya nguo za watoto.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post