Elon Musk apata mtoto wa 11

Elon Musk apata mtoto wa 11

Mmilikiwa mtandao wa X na bilionea kutoka nchini Marekani amethibitisha kupata mtoto wa kiume wa tatu na mpenzi wake Grimes.

Elon ameweka wazi taarifa hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter au X na kuchapisha jina la mtoto huyo ambalo ni Tau au Techno Mechanicus ambalo wengi wameshangazwa nalo kwa jinsi lilivyo la tofauti.

Grimes na Elon tayari wana watoto wengine wawili  ambao mmoja ni wakiume mwenye umri wa miaka mitatu waliyempa  jina la “X  A A-12” huku binti yao mwenye umri wa mwaka mmoja anaitwa “Exa Dark Sideral”.

Hata hivyo tajiri huyo anawatoto wengine kutoka kwa wanawake tofauti tofauti ambao wote kwa ujumla pamoja na mtoto huyo mchanga anakuwa na watoto 11.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags