Elon aishauri Wikipedia kubadili jina

Elon aishauri Wikipedia kubadili jina

Mfanyabiashara na tajiri mkubwa duniani Elon Musk amewashauri wamiliki wa mtandao wa Wikipedia kubadilisha jina lao huku akidai atawapatia ofa ya zaidi ya dola bilioni moja.

Elon kupitia mtandao wake wa X ameandika kuwa atawapa fedha hizo endapo wakikubali kubadili jina hilo. Maoni ya watu mbalimbali yanasema huenda Musk anatamani kuumiliki mtandao huo maarufu kwa taarifa duniani.

Musk anatoa kauli hiyo ikiwa ni miezi michache tangu abadilishe jina mtandao wake wa Twitter na sasa kujulikana kama X.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags