Ed Sheeran ashinda kesi

Ed Sheeran ashinda kesi

Staa wa muziki wa nchini Uingereza Ed Sheeran ameshinda kesi  iliyokuwa ikimkabili ya wimbo wake maarufu wenye zaidi ya views bilioni 3.5 kwenye Youtube “Thinking Out Loud” haukukiuka hakimiliki za wimbo wa mwimbaji wa Marekani Marvin Gaye uitwao “Let’s Get It On.”

Baraza la Mahakama limesema Ed Sheeran alitunga na kutengeneza wimbo wake kwa kujitegemea na hakuna kipengele chochote kwenye utunzi wa nyimbo hiyo kilichotoka kwenye wimbo wa Marvin Gaye.

Kesi ambayo imetrend sana duniani baada ya mashtaka hayo dhidi ya Ed Sheeran kufunguliwa mwaka 2017 ila hatimaye uamuzi ulitolewa mapema jana kuhusu sakata hili ambalo Ed Sheeran aliwahi kuweka ahadi ya kuacha kufanya muziki endapo angekutwa na hatia ya kuiba wimbo wa Marvin Gaye.

Aidha ndugu wa mtunzi mwenza wa nyimbo ya Marvin Gaye walimfungulia kesi Sheeran wakidai kwamba mdundo wa sauti wa nyimbo hizo mbili ulikuwa unafanana wakisema Ed alikiuka hakimiliki ya wimbo yao ambapo kama Ed Sheeran angekutwa na hatia angetakiwa kuwalipa walalamikaji dola milioni 100 kama fidia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags