Dullvann "Atakae muona Pili anipetaarifa"

Dullvann "Atakae muona Pili anipetaarifa"

Mchekeshaji Dullvani ameshikwa na hofu baada ya kutompata kwenye simu mwigizaji mwenzake Gladness maarufu kama Pili kufuatia post 2 alizoweka Instagram akielezea ugonjwa wa afya ya akili ambao umekuwa ukimsumbua baada ya kujifungua.

Dullvani ameandika kupitia ukurasa wake wa instagram akionesha kupata hofu kwani watu wanaweza kuchukulia vitu hivyo kawaida baadae vikaleta madhara.

"Napata wasiwasi sana kutokana na post zake 2 za mwisho alizopost na juzi tulikuwa tunashuti Kitimtim kuna mambo alikuwa anajaribu kunielezea na hichi kinachotokea kwenye page yake ndo nazidi kupata wasiwasi kidogo" ameandika Dullvani.

Hata hivyo Dullvani amesema amekuwa akijaribu kupiga simu kwa Gladness 'Pili' lakini hazipokelewi nakuomba kwa yeyote atakae muona Mchekeshaji huyo atoe taarifa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags