Drake aondoa ngoma aliyotumia sauti ya Tupac

Drake aondoa ngoma aliyotumia sauti ya Tupac

Baada ya mwanasheria wa familia ya Tupac, Howard King kumpa saa 24  rapa Drake kufuta ngoma ya‘ Taylor Made Freestyle’ aliyotumia AI (akili bandia) kutengeneza sauti ya marehemu Tupac, hatimaye mwanamuziki huyo kutoka Canada tayari amefuta wimbo huo kwenye platform za kusikiliza muziki.

Kwa mujibu wa tovuti ya Billboard imeeleza kuwa ilifuatilia platform zote za kusikiliza wimbo huo na kugundua kuwa ngoma hiyo tayari imefutwa siku ya jana Alhamisi Aprili 25.

Kupitia statement iliyotolewa na Mwanasheria huyo ilieleza kuwa siyo uungwana kutumia sauti ya marehemu bila idhini ya familia yake huku akiweka wazi kuwa huu ni unyanyasaji wa wazi kwa moja wa nguli katika muziki wa Hip-hop.

‘ Taylor Made Freestyle’ ni wimbo ambao Drake aliuachia rasmi kwa ajili ya kumchana Kendrick Lamar ambapo alitumia AI kutengeneza sauti ya marehemu Tupac na Snoop Dogg wimbo huo ukiwa kama ni muendelezo wa bifu lao.

Tupac Shakur alizaliwa Juni 16, 1971 na alifariki September 13, 1996 akiwa na miaka 25, huku kesi ya mauaji ya kifo chake bado inaendelea mahakamani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post