Dr Dre kwenye album ya pamoja na Snoop Doggy

Dr Dre kwenye album ya pamoja na Snoop Doggy

Baada ya mwanamuziki na producer kutoka nchini Marekani Dr Dre kutunukiwa nyota ya heshima ya ‘Hollywood Walk of Fame’, ametangaza ujio wa album ya pamoja na ‘rapa’ Snoop Dogg na 50Cent.

Dre ameweka wazi suala hilo kupitia mahojiano yake ya moja kwa moja (live) na Jimmy Kimmel ambapo ameeleza kuwa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha album yake ya pamoja na Snoop itwayo ‘Missionary’ ambayo inatarajiwa kutoka April mwaka huu.

Hii sio mara ya kwanza kwa wawili hao kutoka album ya pamoja, ikumbukwe kuwa mwaka 1993 walitoa album ya pamoja iliyopewa jina la ‘Doggystyle’ ambayo ilivuma zaidi miaka hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags