Djokovic ajiondoa michuano ya Indian Wells

Djokovic ajiondoa michuano ya Indian Wells

Nyota wa tennis Mserbia Novak Djokovic amejiondoa kushiriki kwenye michuano miwili ya Indian Wells na Miami Open 2022 yanayofanyika mjini California nchini Marekani kutokana na sheria za udhibiti wa Uviko 19 zilizopo nchini humo.

Djokovic mwenye umri wa miaka 34 ambaye ni mshindi wa mara 20 wa taji la Grandslam ameshindwa kukidhi vigezo vya ushiriki ambacho kinataka mshiriki kuwa amepata chanjo ya Uviko 19 kwa washiriki ambao sio raia wa Marekani.

"Niombe radhi kwa mashabiki wangu kwamba sitashiriki kwenye michuano ya Indian Wells,sehemu nzuri nipapendapo kucheza na natumaini tutaonana tena mwakani" ameandika Djokovic kwenye mtandao wake wa twitter

Matumaini ya Novak Djokovic yalikuwa kupewa kibali maalumu kutoka idara ya afya ya Marekani CDC ambayo imekataa kulegeza masharti huku nafasi yake ikichukuliwa na nyota kutoka Bulgaria Grigor Dimitrov ilhali kwa Joker hili litakuwa shindano la pili kukosa kushiriki baada ya Australian Open 2022

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags