Dili la Trevor Noah kuitangaza S. Afrika laingia doa

Dili la Trevor Noah kuitangaza S. Afrika laingia doa

Mchekeshaji na mtangazaji maarufu nchini Marekani Trevor Noah ajikuta njia panda baada ya ‘dili’ lake la kuitangaza South Africa kuzua gumzo kwa baadhi ya wabunge na wananchi kudai kuwa pesa wanayomlipa ni kubwa na nchi hiyo haina fedha za kutosha kwa sasa.

‘Dili’ hilo la Trevor lilikuwa ni Randi 33 milioni ambayo ni zaidi ya tsh 4 bilioni za kitanzania kwa video ya dakika 5, kuitangaza South Africa kama kuvutio cha utalii.

Aidha Waziri wa utalii Patricia de Lille amesema kuwa mchekeshaji huyo atalipwa na Baraza la Utalii nchini humo na sio kwa fedha za umma. Huku baadhi ya wadau wameunga mkono pendekezo hilo wakieleza kuwa ushawishi aliyonao Noah unaweza kukuza utalii wa nchi hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags