Diddy bado yupo Marekani

Diddy bado yupo Marekani

Baada ya vyombo vya habari mbalimbali nchini Marekani kudai kuwa mwanamuziki Diddy amekimbilia katika visiwa vya Caribbean, baada ya kuonekana katika uwanja wa ndege wa Opa-Locka, na sasa imebainishwa kuwa ‘Rapa’ huyo hakuwepo kwenye ndege hiyo huku akitajwa kuwa bado yupo Marekani.

Taarifa hiyo inakuja baada ya ndege binafsi ya Diddy kuonekana ikifanya safari za mara kwa mara toka juzi Jumapili huku safari yake ya mwisho ikionekana katika kisiwa hicho cha Caribbean.

Wiki hii imeanza vibaya kwa ‘rapa’ Diddy ambapo siku ya jana Jumatatu Machi, 25 Mawakala wa Usalama wa Taifa walifanya upekuzi wa makazi ya nyota huyo anayehusishwa kwenye madai ya biashara ya ngono.

Aidha mpaka kufikia sasa bado haijabainishwa ni wapi msanii huyo yupo licha ya watoto wake wawili wakiume Justin na King Combs, kukamatwa na askari.
.
.
.
#MwananchiScoop






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags