Diddy afuta posti zote Instagram

Diddy afuta posti zote Instagram

Mkali wa Hip-hop kutoka Marekani Diddy Combs ameripotiwa kusafisha ukurasa wake wa Instagram kwa kufuta posti zote alizowahi ku-share kwenye mtandao huo ikiwemo video yake ya kuomba radhi kufuatia na tukio la kumpiga aliyekuwa mpenzi wake Cassie la mwaka 2016.

Kwa mujibu wa tovuti ya Forbes imeeleza kuwa Diddy alifuta picha pamoja na video zote siku ya jana Alhamis Juni 20 huku ‘akaunti’ yake ikiendelea kushuka ambapo mpaka kufikia sasa ina followers 19.9 milioni.

Diddy amekuwa akiandamwa na kesi za biashara ya ngono na unyanyasaji wa kijinsia tangu Novemba mwaka jana huku aliyekuwa mtayarishaji wa kazi zake Rodney "Lil Rod" Jones akidai kuwa Combs alikuwa akiandaa sherehe za biashara ya ngono.

Hata hivyo kutokana na tuhuma hizo nyumba za ‘rapa’ huyo zilizopo Los Angeles na Miami zilifanyiwa msako na mawakala wa Uchunguzi wa Usalama wa Nchi (HSI).

Aidha licha ya kufunguliwa kesi saba mpaka sasa lakini bado hakuna ushahidi madhubuti wa kumtia nguvuni mwanamuziki huyo huku baadhi ya mastaa akiwemo Suge Knight wakidai kuwa Diddy ni FBI.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post