Diamond: Tumieni changamoto zangu kama motisha

Diamond: Tumieni changamoto zangu kama motisha

Nyota wa muziki wa #bongofleva nchini Diamondplatnumz amewasihi vijana wenzake kutumia changamoto na kheri za maisha yake kama motisha ya kufanikiwa kimaisha.

Diamond ameyaeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram, kuwa anaamini kila kitu kinawezekana chini ya jua ila inabidi wazingatie vitu vichache ambavyo ni utayari, juhudi, uvumilivu, ubunifu, adabu, na zaidi kutokata tamaa.

Diamond alimalizia kwa kueleza kuwa “Vijana wenzangu, huyo kijana unaemuona hapo ni jasiri na mkomavu kwelikweli na ndiyo moja ya nguzo za kuwepo hapo hadi leo, kama yeye anaweza basi naamini sisi wote tunaweza, Mwenyezi Mungu atujaalie Ijumaa ya leo ikawe yenye Kheri na kutufanikisha ndoto zetu wote”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags