Diamond: Sijawa msanii kwa bahati mbaya, punguzeni uchambuzi

Diamond: Sijawa msanii kwa bahati mbaya, punguzeni uchambuzi

Baada ya baadhi ya watu kumsema vibaya Diamond kuhusiana na wimbo wake wa ‘Shu’ kuwa hautofika mbali wala kufanya vizuri, Simba ameendeleza mashambulizi kwa kutolikalia kimya swala hilo na kutoa  majibu.

Kupitia Instastory yake ame-share video ambayo vijana wawili wakicheza amapiano ambazo ni Top 2023 nchini South Africa namba mbili ikiwa ni wimbo wake wa ‘Shu’,  na kuandika ujumbe usomekao,

“Hii #Shu imejua kunidhalilishia watu, jamani mnapoona natoa ngoma punguzeni uchambuzi, maana niwazapo hamuwezi fika na sijawa tuu msanii kwa bahati mbaya, ni mwenyezi mungu alinijalia niwe hivyo, kuna anayonionyesha ambavyo akili yako haiwezi kamwe viona.”
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags